Marehemu Faith enzi za uhai wake
Umati mkubwa wa waombolezaji leo Jumamosi February 21, 2015 wamejumuika na familia ya Mzee Geofrey Gondwe katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele Marehemu Faith Catherine Gondwe, dada yetu aliyeaga dunia ghafla Jumanne iliyopita nyumbani kwao Baahari  Beach jijini Dar es salaam. Ujumbe wa sauti wa kurekodiwa kutoka kwa Mzee Gondwe ambaye yuko India kwa matibabu kuliwaliza wengi na wakati huo huo uliwafariji pale aliposema "Kufariki dunia kwa Faith ni mapenzi yake Mungu"
Ibada ya mazishi ikiendelea
Shada maalumu kwa Faith
Mke wa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathia Chikawe, Profesa Amandina Lihamba akiweka shada la maua kwa niaba ya familia yao ambao ni ndugu wa karibu na familia ya Gondwe
Wanachama wa Jambo Group ambao ni marafiki wa karibu wa baba wa marehemu wakiweka maua kaburini
Marafiki waliosoma na Marehemu Faith nchini India wakiweka maua kaburini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Njia ni moja. Leo umetangulia. Kila mtu ana siku yake. Upumzike kwa Amani. Poleni sana wazazi, ndugu, jamaa na Marafiki wa Faith Catherine Gondwe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...