Karibu sana na asante kwa kujiunga nasi katika kipindi hiki cha HUYU NA YULE
Tumepata fursa ya kuongea na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi
Tumefanya mazungumzo naye ya sehemu nne, kueleza safari yake kimaisha
Na katika sehemu hii ya nne na ya mwisho ya mazungumzo yetu, Mhe Balozi Nyang'anyi anaanza kuelezea
1:Tukio la ugaidi la Septemba 11, 2001 - walivyopata taarifa (kama wanadiplomasia), na kilichofuata
2: Jukumu la kukuza mwanya wa biashara kati ya Marekani na Afrika, ambalo lilisababisha kupitishwa kwa muswada wa sheria wa AGOA
3: Siku yake ya kawaida kama Balozi inavyokuwa na alizimudu vipi?
4: Kituo chake kipya cha kazi huko Abu Dhabi Julai 2002
5: Utata juu ya wajibu wa ofisi za ubalozi kwa wananchi wake
6: Maisha baada ya kustaafu
7: Kazi yake kama Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC)
8: Nani alioshirikiana na kuhusiana nao kwa urahisi zaidi
9: Maisha yake ya kisiasa na BUSARA ZAKE
KARIBU
Kama ulikosa sehemu za awali, unaweza kuangalia Sehemu ya kwanza hapa, sehemu ya pili hapa na sehemu ya tatu hapa
Kwa kweli nime enjoy the whole story ya Mh. Balozi: Mustafa Nyang'anyi. Kwa kweli hayakuwa mahojiano tana, bali ni maongezi, lakini ni yenye kuhamasisha, kutia moyo na kuifunza jamii kwa namna moja ama nyingine, khususan katika masuala mazima ya uongozi na nyadhifa mbali mbali ndani na nje ya nchi. Pia nimefurahi kuskia mbali ya kustaafu kwake, Mh. bado anaithamini na kuijali asili na chimbuko lake la nyumbani 'Kondoa' alikotokea na katu hakuacha kuisifia jamii yake kwa jumla na ambako sasa amekuwa akijishughulisha na shughuli za kilimo. Kadhalika tunashkuru sana kwa nasaha zake kwa aliposema "... katika maisha , uaminifu, kuwa mkweli na kutojiingiza katika matatizo yeyote yanaweza kukuharibia sifa yako..." Hakika ni maneno yenye busara na hekma kwa mwenye kuyazingatia. Mwenyeez Mungu akujaaliye umri mrefu, maisha mema na kila la kheri with your entire family. Pongezi za dhati kwa jopo zima linalounda kipindi hiki cha 'Huyu Na Yule'.
ReplyDelete"OLD IS GOLD", nimemsikiliza huyu mzee wetu mstaafu kwa kweli nimepata mambo mengi sana muhimu ya kujifunza katika maisha..Hongera sana mzee Nyang'anyi nakutakia maisha marefu umenifundisha mengi na mengi nilikua siyajui kuhusu kazi na nchi yetu kwa ujumla...keep it up mzee Nyang'anyi!!
ReplyDeleteMdau wa Oxford,UK.