Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla jana alifanya ziara katika Jimbo lake hilo kwa kutumia usafiri wa pikipiki kufika kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero ambacho kwa historia hakijawahi kufikiwa na kiongozi yeyote tangu uhuru.

Mbunge huyo ambaye amesifika na kuweka rekodi ya kutembelea vijiji vyote 130 vya Jimbo lake hilo,aliona umuhimu kuwafikia wananchi na wana CCM wa Ifumbo kwa njia ya pikipiki ili ajionee changamoto na kuchukua hatua stahiki ili kukabiliana nazo.

Makalla alifika kwenye kitongoji hicho cha Ifumba na kulakiwa kwa shangwe na wananchi wa kijiji hicho ambao walifurika kwa wingi kumpokea, na amehaidi kutuma watalaam wa halmashauri wafike na kuiona barabara na kuingiza katika mipango.

Aidha alikagua ujenzi wa shule ya msingi Ifumbo na kuchangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo,pia amesaidia timu ya Ifumbo Star jezi na mpira na kuwahamasisha kujiandikisha kwenye daftari la wapigakura pindi litakapoanza.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa amepakiwa kwenye pikipiki (Bodaboda) wakati akielekea kwenye kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero. 
Msafara wa Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla kuelekea kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero. 
Walifika kwenye kitongoji hicho muda muafaka kabisa na kuandaliwa chai na magimbi.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akikabidhi baadhi ya vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya vijana wa kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kwa nini Mheshimiwa Makala na dereva wake wa bodaboda hawakuvaa kofia ngumu wakiwa katika usafiri wao huo wa bodaboda?

    ReplyDelete
  2. Hi bro MNichuzi ,nirushie hii comment yangu.Kiongozi ni kioo cha jamii na huyu mh. kutovaa element (Kofia ngumu ) naona imekaa vibaya sana ,hivyo amesahau au hajui kama yeye kama kiongozi ni mfano na kioo cha jamii,yaani twaelekea pabaya!!

    ReplyDelete
  3. AChilia mbali bodaboda na kofia ngumu hiyo ni kwa usalama wake, yaani umbali wote huo kuja kugawa mipira???? na huyu mpiga picha ameogopa hata kutuonesha hadhira jinsi inavyosononeka......Ebu tuwekee ule wimbo mpya wa Mrisho Mpoto wa njoo uchukue tuburudike!!!!

    ReplyDelete
  4. Huyu Naibu Waziri anafikiri aidha (1) Kuwa kiongozi in maana ya kuwa juu ya sharia, au/na (2) Hakuna ulazima kufuata sharia maeneo ya vijijini _ akumbuke ajali haichagui eneo, na kofia ngumu ni kwa faida yake.

    ReplyDelete
  5. Aisee wewe Makalla ni mtu wa watu ndo umeingia juzi tu kwenye ubunge achilia uwaziri umeishafika mpaka kwenye vijiji ambavyo havifikiki kwa sababu hakuna barabara. Aisee inabidi wakupe tena miaka ndo upeleke barabara

    ReplyDelete
  6. Uwe mayu uwe leka maigizo maso yaani ite adani uwe

    ReplyDelete
  7. Kweli ni mwaka wa uchaguzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...