Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla jana alifanya ziara katika Jimbo lake hilo kwa kutumia usafiri wa pikipiki kufika kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero ambacho kwa historia hakijawahi kufikiwa na kiongozi yeyote tangu uhuru.
Mbunge huyo ambaye amesifika na kuweka rekodi ya kutembelea vijiji vyote 130 vya Jimbo lake hilo,aliona umuhimu kuwafikia wananchi na wana CCM wa Ifumbo kwa njia ya pikipiki ili ajionee changamoto na kuchukua hatua stahiki ili kukabiliana nazo.
Makalla alifika kwenye kitongoji hicho cha Ifumba na kulakiwa kwa shangwe na wananchi wa kijiji hicho ambao walifurika kwa wingi kumpokea, na amehaidi kutuma watalaam wa halmashauri wafike na kuiona barabara na kuingiza katika mipango.
Aidha alikagua ujenzi wa shule ya msingi Ifumbo na kuchangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo,pia amesaidia timu ya Ifumbo Star jezi na mpira na kuwahamasisha kujiandikisha kwenye daftari la wapigakura pindi litakapoanza.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa amepakiwa kwenye pikipiki (Bodaboda) wakati akielekea kwenye kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero.
Msafara wa Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla kuelekea kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero.
Walifika kwenye kitongoji hicho muda muafaka kabisa na kuandaliwa chai na magimbi.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akikabidhi baadhi ya vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya vijana wa kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero.
Kwa nini Mheshimiwa Makala na dereva wake wa bodaboda hawakuvaa kofia ngumu wakiwa katika usafiri wao huo wa bodaboda?
ReplyDeleteHi bro MNichuzi ,nirushie hii comment yangu.Kiongozi ni kioo cha jamii na huyu mh. kutovaa element (Kofia ngumu ) naona imekaa vibaya sana ,hivyo amesahau au hajui kama yeye kama kiongozi ni mfano na kioo cha jamii,yaani twaelekea pabaya!!
ReplyDeleteAChilia mbali bodaboda na kofia ngumu hiyo ni kwa usalama wake, yaani umbali wote huo kuja kugawa mipira???? na huyu mpiga picha ameogopa hata kutuonesha hadhira jinsi inavyosononeka......Ebu tuwekee ule wimbo mpya wa Mrisho Mpoto wa njoo uchukue tuburudike!!!!
ReplyDeleteHuyu Naibu Waziri anafikiri aidha (1) Kuwa kiongozi in maana ya kuwa juu ya sharia, au/na (2) Hakuna ulazima kufuata sharia maeneo ya vijijini _ akumbuke ajali haichagui eneo, na kofia ngumu ni kwa faida yake.
ReplyDeleteAisee wewe Makalla ni mtu wa watu ndo umeingia juzi tu kwenye ubunge achilia uwaziri umeishafika mpaka kwenye vijiji ambavyo havifikiki kwa sababu hakuna barabara. Aisee inabidi wakupe tena miaka ndo upeleke barabara
ReplyDeleteUwe mayu uwe leka maigizo maso yaani ite adani uwe
ReplyDeleteKweli ni mwaka wa uchaguzi
ReplyDelete