Mdau Christopher Simon Suday (MC Mwakitwange - Chotala) akiwa ameshikana mkono na mai waifu wake Bi. Neema Suday wakati wakifungishwa ndoa na Mhashamu Askofu Dr. Chilongani wa kanisa kuu la Anglicana dayosisi ya Central Tanganyika mjini Dodoma hivi karibuni. maharusi hao wote wa wakazi wa mji wa Dodoma.Baada ya Maharusi hao kumeremeta kwao kanisani hapo,walienda kutoa sadaka katika kijiji Cha Matumaini cha Mtakatifu Gaspar cha watoto yatima, na baadae kumalizia na sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa LandMark Kilimani mjini Dodoma.
Maharusi Christopher Simon Suday (MC Mwakitwange - Chotala) na mai waifu wake Bi. Neema Suday wakiwa kanisani kuendelea na ibada ya ndoa yao.nyuma yao ni Bestman wa Bwana harusi.
Christopher Simon Suday (MC Mwakitwange - Chotala) akimwaga wino kwenye cheti cha ndoa kwa furaha tele huku mamsapu wake akimcheki.
Sasa wote ni mwili mmoja.
Maharusi Christopher Simon Suday (MC Mwakitwange - Chotala) na mai waifu wake Bi. Neema Suday wakiwa kwenye picha ya pamoja na wapambe wao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...