Mchezaji wa timu ya Yanga,Mrisho Khalfan Ngassa akiwania mpira na Mchezaji wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo.Yanga imeshinda bao 2 - 0 zilizotiwa kimiani na Mshambuliaji Hamis Tambwe dakika ya kwanza ya mchezo na 55. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Golikipa wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana akiondosha hatari iliyokuwa ikielekezwa langoni mwake wakati wa Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo.Yanga imeshinda bao 2 - 0.
Winga machachari wa Yanga,Saimon Msuva akiangalia namna ya kumtoka beki wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana,Othusitse Mpharitlhe wakati wa Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika ulipigwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo.Yanga imeshinda bao 2 - 0.
Beki wa Yanga,Mbuyu Twite akirusha mpira kwa ustadi mkubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...