Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (mwenye kilemba kichwani) akimsikiliza Afisa Mtendaji wa Kata ya Msalato Dodoma Ndg. Herman Malindira (kulia) akiwasilisha taarifa ya mradi wa ujenzi maabara kwenye sekondari ya Chikole Feb. 16, 2015.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kushoto) akitoa maagizo kwa viongozi wa Manispaa ya Dodoma na kata ya Msalato baada ya kutoridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa maabara wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Mjini Dodoma Feb. 16, 2015.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (katikati) akionesha kutokuridhishwa na hatua ya ujezi wa maabara kwenye sekondari ya Miyuji inayojengwa na Kata za Miyuji na Mnadani ikiwa hatua ya msingi wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Mjini Dodoma Feb. 16, 2015, Amemuagiza Mkurugenzi Manispaa ya Dodoma kuwachukulia hatua watendaji wote walioshindwa kusimamia ujenzi wa maabara.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (katikati) akiwaagiza viongozi wa Manispaa ya Dodoma na kata ya Chamwino kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa maabara sekondari ya Chinangali ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili, Mhe. Gallawa ameonesha kutokuridhika na ujenzi wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Mjini Dodoma Feb. 16, 2015 na kukuta maabara ik kwenye hatua ya ujenzi wa msingi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kushoto) akiwaagiza viongozi wa Manispaa ya Dodoma na kata ya Chang’ombe kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa maabara sekondari ya Lukundo ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili, Mhe. Gallawa ameonesha kutokuridhika na ujenzi wa Maabara Manispaa ya Dodoma wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Feb. 16, 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Waajibishe mkuu wanakaa kula hela za walipa kodi bure.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...