Mbunge wa Jimbo la Chalinze  na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya  Chama cha  Mapinduzi Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa  katika picha ya   pamoja na  Muwakilishi wa Kudumu wa Jamburi ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako  Manongi  (kushoto) na  Naibu Mwakilishi wa  Kudumu,  Balozi Ramadhan Mwinyi. Mhe Ridhiwani Kikwete ( Mb)  alikuwa Jijini New York kwa ziara ya kikazi ambapo pia  alikuwa mgeni  rasmi  katika  hafla ya  miaka 38 ya  kuzaliwa kwa  Chama cha Mapinguzi iliyoandaliwa na Tawi la CCM New York na vitongoji vyake.
Mhe. Ridhiwani Kikwete ( Mb) akiwa  katika picha ya pamoja na  Mabalozi   na  baadhi ya  maafisa wa Uwakilishi wa  kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. Mhe.  Ridhiwani Kikwete  pamoja na  kuhudhuria hafla ya   CCM kutimiza miaka 38 pia alipata fursa ya kufika katika Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika  Umoja wa Mataifa, fursa aliyoitumia  kubadilishana  mawazo  na   Maafisa wa Uwakilishi.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...