Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia mauaji ya Kimbari ya Rwanda (UN-ICTR) yenye makao yake makuu mjini Arusha imekabidhi msaada wa vifaa vya ki-eletronic vinavyosaidia kuongeza ufanisi wa kazi za kimakahakama kwa Jaji Mkuu wa Mahakama Tazania Mhe. Othman Mohamed Chande katika sherehe fupi iliyofanyika mahakamani hapo Arusha.
Vifaa hivyo ni pamoja na mashine 19 ziitwazo Dictaphone Machines na mashine nyingine 19 ziitwazo Transcribers.
Viffaa hivyo vilikabidhiwa na Kaimu Mkuu wa Utawala wa UN-ICTR Bwana Emmanuel Kodwo Bartels. Vifaa hivyo vilikuwa vikitumiwa na UN-ICTR katika kazi zake za kila siku. Mahakama hiyo inamaliza kazi zake mwaka huu.
Vifaa hivyo vikiwa vipya hununuliwa kwa US$ 5000 (Sh 9 millioni) kila kimoja.
UN-ICTR imebakiza kesi moja tu ambayo itamaliziwa kabla ya mwisho wa mwaka huu. Kesi dhidi ya watuhumiwa 93 zimeshamalizwa na mahakama hiyo.
Kesi hizo zilijumuisha watu wazito nchini Rwanda wakiwemo mawaziri akiwamo waziri mkuu, wakuu na makamanda wa majeshi, wakuu wa mikoa na wilaya, waandishi waandamizi, wakuu wa madhehebu ya dini na wafanyabiashara wakubwa.
Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman akipokea kifaa kimoja kutoka kwa Bw. Bartels (menye miwani). Wanaoshuhudia ni viongozi wa mahakama hizo mbili wakiwemo (kutoka kushoto) Bw. Danford Mpumilwa, Afisa Habari wa UN-ICTR na Bw. Saidou Guindo, Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa UN-ICTR. Kutoka kulia ni Mama Margaret Shaidi-Ngatunga akifuatiwa na Bw. Richard Lipscombe, kutoka kitengo cha Ugavi cha UN-ICTR. Mwingine ni Bw. Jerry Mburi, Afisa Sheria wa UN-ICTR ( wa nne kulia).
Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. John Kahyoza akiweka saini kupokea vifaa hivyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...