
Ayobami ni mwimbaji ambaye anafanya vizuri katika muziki huo
wa Kumtukuza Mungu kupitia nyimbo mbalimbali.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex
Msama alisema katika taarifa yake kuwa mwaka huu wanataka kutoka kivingine.
“Mashabiki wamekuwa wakiomba tumualike Ayobami, bado tunapokea
maoni mbalimbali na kulingana na vigezo vyetu tutajipanga,” alisema Msama. Alisema kwa kuwa wameamua kukuza muziki huo hapa nchini, wataalika
wasanii mbalimbali wa kimataifa ili kulifanya tamasha la mwaka huu liwe la aina
yake.
Alisema wamekuwa wakiwatumia katika matamasha yake
yaliyoasisiwa tangu mwaka 2000, waimbaji kutoka Kenya, Zambia, Afrika Kusini,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na wa hapa nchini.
“Niliyoeleza mwanzoni yanakamilika, kwa sababu nilidhamiria kuliboresha
zaidi Tamasha la Pasaka kwa kuwashirikisha waimbaji wa Kimataifa, mashabiki
wakae mkao wa kula kupata ladha tofauti katika tamasha la mwaka huu,” alisema
Msama.
Baadhi ya waimbaji waliopata kutumbuiza Tamasha la Pasaka
tangu lianzishwe ni Rebecca Malope, Keke Phoofolo (Afrika Kusini), Ephraim
Sekereti (Zambia), Faraja Ntaboba (DRC) na Sarah K, Paul Mwai (Kenya).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...