ASSALAM ALAIKUM WARAHMATUL LWAHI WABARAKAATUH
Coventry Muslim Swahili Association (COMSWA) inayo furaha kuwatangazia kuwa Sheikh mwenye ushawishi mkubwa Tanzania na nje ya Tanzania, Sheikh Muhammad Eid (Abu Eid) yuko nchini Uingereza (United Kingdom) katika ziara ya kida’wa.
Siku ya Ijumaa 13/02/2015 atazungumza na Waumin baada ya swala ya Al jumaa kenye ukumbi wa Al madrasatul Munawarah mjini Coventry kwenye Anuani 88 Paynes Lane, Coventry, CV1 5LJ, UNITED KINGDOM.
Jumamosi tarehe 14/02/2015 atazungumza na Waumin kwenye ukumbi wa Muslim Resource Centre, Coventry, CV6 5EE, United Kingdom. Nasaha hizo zitatolewa ktk shughuli maalum (Fundraising Buffet Dinner) iliyoandaliwa ili kukusanya michango kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti, Madrasah na kituo cha jamii. Shughuli itaanza saa saba mchana hadi saa mbili usiku ambapo masheikh kutoka sehemu mbalimbali watatoa nasaha zao.
Pamoja na mambo mengine malengo hasa ya jumuiya ni kuikusanya jamii pamoja ili iweze kusaidiana kufanya mambo yao kwa ufanisi na kuamrishana mambo mema. Wote mnakaribishwa na kwa maelezo zaidi kuhusu shughuli yenyewe, maasiliano na shughuli za COMSWA tembelea www.comswa.com.
"Wote mnakaribishwa", hata sisi wamisionari? maana na hamu ya kuja kupata mawaidha toka kwa sheikh, sasa weka bayana kama wamisionari twawez kuja kupata nasaha na ubwabwa.
ReplyDeleteMdau mmisionari- Coventry.