Ndegevita moja ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiteketea kwa moto huku jitihada za kuuzima zikiendelea katika ajali iliyotokea leo Februari 27, 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.

Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita,  Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto. 

Hata hivyo, rubani wa ndegevita hiyo Meja Peter Lyamunda  alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya kawaida .

Wananchi wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama kawaida na kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala miundo mbinu. 


Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa eneo la tukio kuangalia mabaki ya ndegevita hiyo iliyopata ajali leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Nafikiri si sawa katika maswala ya usalama wa nchi kuonyesha picha ambazo zinatoa details za vifaa vya kivita vya nchi husika.

    Nashauri blog hii ya Michuzi na wahusika waliopiga picha wajaribu kulizingatia swala hili.

    Samweli.

    ReplyDelete
  2. Hizo ndege sijui zitakuwa zimebaki ngapi! Tunahesabu maumivu..

    ReplyDelete
  3. The mdudu, pole zangu nyingi sn sn kwenu jeshi langu jwtz..nimeumia sn moyoni kwakuipoteza hii ndegevita but as long as mjeshi wetu umepona basi tujipange vizuri ili ndugu zetu wachina watupatie mnyama mwingine haraka iwezekanavyo.

    ReplyDelete
  4. Kulikuwa hakuna haja ya picha ya ndegevita kuwekwa hadharani kwa usalama

    ReplyDelete
  5. Wananchi wala shaka hatuna baridi kama maji ya mtungi, kwa lipi hasa mpaka tuwe na shaka??na hawa wanaosema picha zisingeoneshwa sijui wa wapi hawa?? ili iweje ndio kumficha details adui ???kwikwikwi.....mnacheza kweli ungetathmini vp ukubwa wa ajari kama ungeletewa taarifa ya imla???ni kutokana na picha za mabaki ndio tunatoa pongezi zetu kwa askari aliyenusurika kwa umahili alioutumia kujiokoa.....

    ReplyDelete
  6. Picha ziko kibao kwenye google, nyie mnaogopa nini? Acheni ushamba usalama upo kibao kwani unafikiri jeshi halikipitia hiyo protocol? Ndege iliyoshiriki kwenye uperation ya Osama ilipigwa picha usalama wake ukoje hapo! Haya mi napita......

    ReplyDelete
  7. Hakika mungu nimwema juu ya Tanzania,kwaufasaha naukuu wakazi yake juu ya viongozi wakuu nawajwshi wenyewe kwakuonyesha jinsi mlivyo bobea katika kazi.kwani mambo haya tumezowea kuyaona kwenye Tv nakuyasikia kwenye vyombo vya habari kua hua watu wanaruka kutoka katika ndege hakika kumbe yapo hata tz.asante yesu kwakuweka mashujaa juu ya nchi yetu.bwana akutie nguvu nakukuponya haraka meja Lyamunda.by Evrin Peter in Majohe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...