“NILIAMUA
kuanzisha Msama Promotions baada ya kuona muziki wa Injili umesahaulika
na unashuka thamani yake.“Hivyo kwa kushirikiana na wenzangu nikaona ni
busara kuuinua ili tuwe kama wenzetu Afrika Kusini ambao wana waimbaji
wa nyimbo za Injili wanaotamba kama Rebecca Malope, Itani Madima, Steve
Kekane, Vuyo Mokoena na wengine wengi,” hiyo ni kauli ya Mkurugenzi wa
Msama Promotions, Alex Msama.
Msama
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka,
anasema alitaka watu wajue na kutambua kuwa muziki wa Injili
unaweza kupigwa kama burudani katika kumbi mbalimbali za starehe na
kuondoa dhana potofu kwamba muziki huo wa Injili haufai kupigwa katika
kumbi hizo.
“Kupeleka
muziki wa Injili kwenye kumbi ambazo hupigwa muziki wa miondoko mingine
ya kidunia si dhambi kama baadhi ya watu wanavyofikiri,”
anasema.Anasema ni zaidi ya miaka 15 tangu walipoanzisha Tamasha la
Pasaka wakati wa sikukuu hiyo kila mwaka na sasa jamii imelikubali na
limekuwa gumzo kubwa kwa jamii.
Anasema
pia dhamira yao nyingine ya kuanzisha tamasha hilo ilikuwa kusaidia
jamii kwa namna mbalimbali kutokana na fedha za viingilio, lakini pia
kuwapa ajira vijana kutokana na tamasha hilo.“Ninachoweza kusema ni
kwamba mwaka huu tumedhamiria kwa dhati kusaidia jamii kwa namna
mbalimbali kutokana na fedha zitakazopatikana kwenye viingilio vya
tamasha.
“Haitakuwa
mara ya kwanza kwetu kusaidia, tumefanya hivyo miaka ya nyuma na
tutaendelea na juhudi hizo kila tutakapopata nafasi ya kufanya hivyo, “
anasema.Anatolea mfano kuwa miaka ya nyuma wamesaidia watu mbalimbali
ikiwemo waathirika wa mabomu yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi Gongo la
Mboto, Dar es Salaam. Pia anasema wamepata kutoa fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji ya biashara wanawake wajane.
Msama
anabainisha kwamba kutokana na dhamira hiyo, ndiyo maana wamekuwa
mstari wa mbele kuandaa matamasha ya muziki wa Injili, lengo likiwa ni
kusaidia masuala mbalimbali.Anasema mwanzoni wakati wanaanza tamasha
hilo mwaka 2000, wamewahi kuandaa matamasha kwenye ukumbi wa
Diamond Jubilee kwa ajili ya kuchangia watoto yatima wa mikoa ya
Morogoro na Pwani, ambao wazazi wao walifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi,
ambapo yote waliyopanga yalifanikiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...