Balozi wa Iran nchini Tanzania,Mh.Mehdi Aghajafari akimpokea Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb) alipowasili katika hafla ya kusherehekea siku ya Taifa la Iran iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi huyo Jijini Dar es Salaam jana usiku.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb) akizungumza mbele ya wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla ya siku ya Taifa la Iran iliyofanyika kwenye makazi ya balozi wa Iran Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Syria nchini, Mhe.Abdulmonem Annan (kushoto) Jaji mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) na Balozi wa Yemen nchini, Mhe.Abdulla Hassan Alamri wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi kwenye hafla ya Siku ya Iran, Naibu waziri Dkt. Mahadhi.
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahaya (kulia) akiwa na Maafisa kutoka Wizara hiyo Bw. Mkumbwa Ally (kushoto) na Bw. Leonce Bilauri (katikati) wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri (hayupo pichani) katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akisalimiana na Balozi wa Syria nchini Mhe. Abdulmonem Annan kwenye sherehe hizo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...