BENKI ya NMB imeanza kutoa huduma zake kupitia mawakala wa MaxMalipo kwa mafanikio katika hatua ya majaribio inayoendelea Kigamboni – Dar es Salaam, Dodoma na Arusha.
Huduma hiyo inayojulikana kama NMB Wakala itakuwa inapatikana kwenye maduka ya kawaida yenye huduma za MaxMalipo, inategemewa kusogeza huduma za benki hiyo mpaka vijijini na kuwa benki ya kwanza kuweza kupenya maeneo ya vijijini.
Kwa ajili ya kuhakikisha huduma hii inawafikia wengi, NMB inafanya matangazo katika eneo la kigamboni kuhamasisha wakazi wa eneo hilo wanapata elimu Zaidi ya jinsi ya kutumia huduma ya NMB wakala. Katika promosheni hii mwananchi yeyeote anaweza kufungua akaunti na kupata Kadi ya ATM papo hapo.
Kwa sasa NMB imemaliza kufanya majaribio katika eneo la Kigamboni – Dar es Salaam kwa mafanikio makubwa na hivyo kuwa tayari kuanza kutoa huduma hiyo nchi nzima huku malengo ya awali ikiwa kuwa na mawakala Zaidi ya ya 3,000 nchi nzima.
Mkazi wa kigamboni akipata maelezo kutoka kwa ofisa wa NMB jinsi anavyoweza kupata huduma ya kibenki kutoka kwa wakala wa NMB kwa kupitia kwa mawakala wa Max malipo na huduma ya NMB Wakala.
Wasanii wakiwatumbuiza wananchi wa Kigamboni katika tamasha la kuelimisha matumizi ya huduma ya NMB Wakala.
ofisa wa NMB akitoa maelezo ya namna ya kupata huduma za NMB kwa kutumia mashine la MaxMalipo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...