Benki bora Tanzania (NMB) imekabidhi hundi ya udhamini wa shilingi milioni 10 kwa mfuko wa pensheni kwa jamii - PSPF kwa ajili ya kufanikisha mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wa mfuko huo.
Mkurugenzi mkuu wa PSPF amewashukuru NMB kwa kuwa karibu Zaidi na wadau wao kwa vitendo tofauti na benki zingine, kwani hundi hiyo ni kielelezo tosha cha benki inayowajali wateja wake.
NMB ni benki bora Zaidi nchini ikiwa na matawi Zaidi ya 170 na mashine za ATM Zaidi ya 600 huku ikijivunia wateja Zaidi ya milioni 2 na ubunifu wa bidhaa zinazomlenga mteja Zaidi kama NMB Wakala, akaunti za Chap Chap na NMB Mobile.
Katika mkutano huo na PSPF, NMB imeweka mabanda yake ya maonyesho na kuonyesha huduma mbalimbali zinazotolewa na benki huku huduma yao Mpya ya NMB Wakala na Chap Chap Instant Account zikiwa ndizo huduma zilizopendwa Zaidi na washiriki wa mkutano huo.
Afisa Mkuu wa kitengo cha biashara ya jumla wa NMB Ndugu
Richard Makungwa, (Kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya
shilingi milioni 10, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF - Adam
Mayingu. Katikati ni Meneja Mwandamizi wa kitengo cha biashara za
Kitaasisi NMB Noela Kivaria.
Afisa Mkuu wa kitengo cha biashara ya jumla
wa NMB Ndugu Richard Makungwa (Kulia)
pamoja Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF - Adam Mayingu, wakiashiria ushirikiano wa
taasisi mbili kwa kugongesha
vinywaji vyao wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na NMB kwa wadau wa PSPF.
Maofisa wa NMB wakifuatilia jambo la muhimu wakati wa hafla hiyo ya PSPF
iliyofadhiliwa na Benki ya NMB.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...