Mkaazi wa Kyela mkoani Mbeya Bwana Edom Dickson Mwansasu amekabithiwa gari aina ya Toyota IST na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mara baada ya kuibuka mshindi kupitia droo ya wiki ya pili ya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi iliyofanyika siku ya ijumaa iliyopita
 Bwana Edom Mwansasu mwenye umri wa miaka 40 anajishughulisha na shughuli za kilimo huko Ngonga Kyela Mkoani Mbeya ameibuka mshindi baada ya kununua na kujiunga na vifurushi vya siku vya huduma ya Airtel yatosha kila siku. 
 Akiongea baada ya kukabithiwa gari bwana Edom Mwansasu alisema ninafuraha sana kuwa mshindi na kutumiza ndoto yangu ya kumiliki gari. Nilipopigiwa simu sikuamini kuwa nimeshinda gari , nilifurahi sana nakupasha habari kwa familia yangu. Sijawahi kumiliki gari hivyo najisikia furaha sana Airtel kunizawadia mimi hii gari kupitia hii promosheni ya Airtel yatosha. Kwa kupitia gari hili sasa na uhakika wa usafiri mimi pamoja na familia yangu lakini pia litanisaidia katika kazi yangu ya kilimo na kuniwezesha kusafirisha mazao yangu kirahisi ukilinganisha na awali nilikuwa natumia baskeli au kukodi gari. 
 ‘Nawapongeza sana Airtel na nawashauri watanzania kuendelea kutumia huduma ya Airtel yatosha na kuamini kuwa nao wanaweza kubahatika na kushinda kama mimi” aliongeza Mwansasu Kwa upande wake Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Bwana Hemed Msangi alisema” kwanza kabisa napenda kuwapongeza Airtel kwa kuanzisha promosheni hii kabambe inayowawezesha watanzania kutoka sehemu mbalimbali kujishindia magari. 
" Naamini kwa kupitia promosheni hii mtawawezesha watanzania wengi kujikwamua kiuchumi na kuwawezesha kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi kirahisi na kwa ufanisi zaidi. Nawapongeza washindi wote waliopatikana mpaka sasa. Lakini natumia fulsa hii kuwaomba wananchi wadumishe amani maana kama sio amani tulionayo basi promosheni kama hizi zisingeweza kufanyika” 
 Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja biashara wa Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushi Alisema” promosheni hii ya Airtel yatosha zaidi ni mahususi kwa wateja wetu Tanzania nzima wanaotumia huduma hii ya Airtel Yatosha kuweza kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku . kujiunga na vifurushi vya Airtel yatosha mteja anatakiwa kupiga *149*99# au kwa kununua vocha vya Airtel yatosha au kununua kupitia huduma ya Airtel Money na kuunganishwa moja kwa moja kwenye droo itakayomwezesha kushinda.
 Mpaka sasa washindi 10 wamepatika ambapo kati yao wawili wanatoka kanda ya nyanda za juu kusini na leo tunamkabithi mshindi wetu wa Mbeya Bwana Edom Mwansansu gari lake na kisha tutamkabithi mshindi wa mkoa wa sumbawanga bwana Saidi Mashiko ambaye ni mganga wa tiba za jadi na mkazi wa Katavi hivi karibuni” 
 “Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kujiunga na vifurushi hivi vya Airtel yatosha na kupata nafasi ya kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku”. Aliongeza Mushi Washinde wengine waliojishindia Toyota IST toka promosheni hii ianze ni pamoja na Ramadhani Dilunga mkazi wa Pwani, Namtapika Kilumba Mkazi wa Mtwara, said Mashiko mkazi wa katavi, Hamim Yoyo mkazi wa Korogwe Tanga, Esther Mashauri Mkazi wa Mwanza, Ibrahim Kimondo mkazi wa Kondoa pamoja na Mwajabu Churian, Sakina Libwana na Justin Wilium wote wakazi wa Dar
Mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu  mkazi wa Kyela Mbeya akitambulishwa  na Meneja biashara wa Airtel  Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushibaada ya kuibuka moja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi
 Kamanda mkuu wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Bwana Hemed Msangi (wa pili kulia)  akimkabithi mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu  mkazi wa Kyela Mbeya baada ya kuibuka moja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. pichani kulia  ni mke wa Edom Mwansasu na kushoto  ni Meneja biashara wa Airtel  Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushi
 Mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu  akiwasha gari mara baada ya kukabithiwa gari lake baada ya kuibuka moja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi.
 Mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu  akiwa ndani ya gari pamoja na mke wake baada ya kukabithiwa gari lake kufatia kuibuka kuwa mshindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi katika droo iliyofanyika ijumaa iliyopita
Sehemu ya magari kibao yanayongoja kunyakuliwa na washindi wa kila wiki wa Airtel hatosha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...