Rais wa Shirikisho la Ujerumani Bwana Joachim Gauck anatarajiwa kuwasili Zanzibar leo asubuhi kwa kufanya ziara ya kutwa moja akitokea Mjini Dar es salaamu. 
Bwana Joachim atapokewa na Mwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein, Mawaziri wa Serikali, Viongozi wa Kisiasa na baadhi ya raia wa Ujerumani waliopo Zanzibar huko Bandari ya malindi Mjini Zanzibar. 
Matayarisho ya mapokezi ya ujio wa Kiongozi huyo wa Shirikisho la Ujerumani yamekamilika ambapo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata wasaa wa kufika Bandari ya Malindi kukagua matayarisho hayo. 
Mshauri wa Rais wa Zanzibar anayesimamia Uchumi, Uwekezaji na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Moh’d Ramia Abdiwawa alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba hatua zote zilizopangwa kuchukuliwa katika matayarisho hayo zimetekelezwa kwa mafanikio makubwa. Balozi Ramia alisema Mgeni huyo anatazamiwa kuwasili kwa Boti iendayo kwa Kasi ya Kilimanjaro wakati wa asubuhi na kupata fursa ya kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein Ikulu Mjini Zanzibar. 
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Zanzibar Balozi Silima Kombo Haji alimueleza Balozi Seif kwamba utaratibu maalum umeandaliwa kwa Viongozi wenyeji waliopangwa kumpokea Kiongozi huyo. Balozi Silima alisema maafisa wa Itifaki watakuwepo Bandarini hapo kwa lengo la kuwaelekeza Viongozi wote waliopangwa kufika eneo hilo kwa shughuli hiyo muhimu ya Kimataifa. 
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alielezea kuridhika kwake na hatua za maandalizi hayo na kuipongeza Kamati maalum iliyoundwa ya kuratibu mapokezi hayo. 
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Bwana Joachim Gauck awapo Zanzibar pia anatarajiwa kufanya mazungumzo na Viongozi wa Kidini katika Hoteli ya Serena iliyopo Forodhani Mjini Zanzibar. Bwana Joachim anatazamiwa kuondoka Zanzibar kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume Zanzibar wakati wa jioni kuelekea mkoani Arusha kumalizia ziara yake Nchini Tanzania.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitembelea Bandari ya Malindi kuangalia matayarisho ya ujio wa  Rais wa Shirikisho la Ujerumani Bwana Joachik Gauck.Kushoto ya Balozi Seif ni Mshauri wa Rais anaesimamia Uchumi, Uwekezaji na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Moh’d Ramia na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Nd. Abdulla Juma Abdulla.
 Balozi Seif akiwa na Viongozi wa Kamati ya kuratibu Mapokezi ya Rais wa Ujerumani wakirudi kukagua eneo la kushukia boti  ziendazo kwa kasi katika Bandari ya Malindi. Kushoto yake ni  Mshauri wa Rais Balozi Moh’d Ramia, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo Haji pamoja na Mkurugenzi Bandari Nd. Abdulla Juma.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa pamoja na Balozi Mdogo wa Heshima wa Shirikisho la Ujerumani hapa Zanzibar Balozi
Has –Dieter Allgaier wakielekea kukagua chum,baa cha watu Mashuhuri { VIP }  kiliopo Bandari ya Malindi ambacho kimewekwa hakiba kwa ujio wa Rais wa Shirikisho la Ujerumani Bwana Joachim Gauck.
Mshauri wa Rais anayesimamia Uchumi,Uwekezaji na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Moh’ d Ramia akimuelezea Balozi Seif hatua zilizochukuliwa katika matayarisho ya ujio wa Rais wa Ujerumani. Kati kati yao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d na kulia ya Balozi Ramia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo Haji. Picha na OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...