Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar akitia saini katika kitabu cha wageni katika ofisi ya kata ya Siela Sing'isi alipotembelea katika kijiji hicho cha Sing'isi.
Mpima wa Halmashauri ya wilaya ya Meru ,Seveline Luambano akiwaonesha wananchi wa vijiji vya Sing'isi na Malala,mipaka pamoja na michoro ya ramani ya eneo la hekari 92 zilizotolewa kwa vijiji hivyo .zoezi hilo limeshuhudiwa na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar.
Mbunge Nassari akiwaongoza wananchi wa vijiji vya Sing'isi na Madiira wakitembelea shamaba la Madiira kutizama mipaka ya eneo la Hekari 92 lililotolewa kwao.
Mbunge Nassari akimsikiliza Mwenyekiti wa kijiji cha Sing'isi  Elishiria Kimoto akitoa maelezo ya kusitishwa kwa zoezi la kuoneshwa eneo hilo hadi pale Maofisa Ardhi wa Halamashauri hiyo watakapo weka mionundo mbuni ya barabara katika eneo hilo.
Mbunge Nasari akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo mara baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya eneo la Shamba la Madiira ambao aliwataka kusitisha kilimo ili kuruhusu maofisa Ardhi kupitishwa greda kwa ajili ya kuchonga barabara pamoja na mitaa katika eneo hilo.
Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...