Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Semamba Makinda (Mb), kwa niaba
ya Bunge la Jamhuri ya Muungao wa Tanzania anatuma salaamu za rambirambi kwa
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Bwana Othman Rashid, kufuatia
kifo cha mama yake mzazi, BI. TAJIRI
ABDALLAH KITENGE, kilichotokea tarehe 5 Februari, 2015.
Aidha, Spika Makinda anatuma salaamu za rambirambi kwa Jaji Mkuu
Mstaafu wa Tanzania Mhe. Augustino Ramadhani kufuatia kifo cha mama yake mzazi,
BI. BRIDGET RAMADHAN, kilichotokea
Februari 3, 2015.
“Nimepokea taarifa za misiba hii kwa masikitiko makubwa na ninawapa
pole familia, ndugu, jamaa na marafiki wote. Ninamwomba Mwenyezi Mungu awape
faraja wafiwa katika kipindi hiki kigumu.
BWANA alitoa na BWANA ametwaa, Jina la BWANA lihimidiwe. Amina.”
Imetolewa na Ofisi ya
Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa
Umma na
Uhusiano wa Kimataifa
DODOMA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...