Wataalam wa Sekta ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Shirika la Umeme nchini (Tanesco), wakiongozwa na Kamishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kushoto), wakiwa katika mazungumzo na wawakilishi wa Kampuni ya Sunshine Group Ltd (Kulia). Mazungumzo yalifanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam na yalihusu uanzishwaji wa Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa ajili ya kusambaza umeme nchini.
Ujumbe kutoka Kampuni ya Sunshine Group Ltd, ukiwa katika mazungumzo na wataalam wa Sekta ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Shirika la Umeme nchini – Tanesco (hawapo pichani). Kampuni hiyo iliwasilisha mapendekezo (proposal) ya kuanzisha Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa ajili ya matumizi ya hapa nchini.
Mtaalam wa Sekta ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Leonard Masanja (wa kwanza Kulia) akichangia hoja katika kikao baina ya Wataalam wa Wizara na wawakilishi wa Kampuni ya Sunshine Group Ltd, Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Majadiliano yalihusu uwezekano wa Kampuni hiyo kuanzisha Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa matumizi ya kusambaza umeme nchini. Wa kwanza Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga.
Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga (Kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sunshine Group Ltd, Bw. Sun Tao aliyekuwa akitoa ufafanuzi wa jambo fulani, mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina ya Wataalam wa Wizara na wawakilishi wa Kampuni hiyo kuhusu uwezekano wa kuanzisha Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa ajili ya kusambaza umeme nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...