WAZIRI wa Uchukuzi,
Samuel Sitta ameelezea kufurahishwa na waandaaji wa Tamasha la Pasaka na kusema
kuwa katika miaka 15 ya tamasha hilo wana mengi ya kujivunia.
Taarifa kwa vyombo
vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na kusainiwa na Mwenyekiti wa Kamati
ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa kamati yake imepokea
salamu kutoka kwa Waziri Sitta akizungumzia maandalizi ya miaka 15 ya tamasha hilo.
“Ni tamasha lenye
tija kwa Watanzania, mimi mwenyewe nimekuwa shahidi wa namna mnavyosaidia
yatima, wajane na makundi mbalimbali ya kijamii.
“Nimesikia mwaka huu
mna tamasha kubwa la miaka 15 tangu muanze kufanya Tamasha la Pasaka, niwatakie
kila la heri katika maandalizi na naamini litakuwa tamasha la aina yake,”
alisema Msama katika taarifa yake akimnukuu Sitta.
Alisema wamekuwa
wakipokea salamu kutoka kwa wadau mbalimbali wakizungumzia kuhusiana na
maandalizi ya Miaka 15 ya Tamasha la Pasaka na wakielezea pia mafanikio
mbalimbali yaliyopatikana kwa kipindi hicho.
Baadhi ya walioguswa
na maandalizi ya tamasha hilo ni waimbaji mahiri wa muziki wa Injili kutoka
Afrika Kusini Solly Mahlangu ‘Obrigado’ na Rebecca Malope.
Wasanii hao wamewahi
kwa nyakati tofauti kuja nchini katika Tamasha la Pasaka, ambapo mwaka huu
waandaji wamepanga kufanya sherehe ya Miaka 15 ya Tamasha la Pasaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...