Home
Unlabelled
PLEASE STOP KILLING OUR DEAR BROTHERS & SISTERS WITH ALBINISM!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Acha kuua na kukata mikono ya albino!.
ReplyDeleteHate people who killings innocent
ReplyDeleteKengereza si hamkitaki jamani, sasa na hapa mnawandikia kwa kingereza wataelewa? wandikieni hicho kiswahili. labda ndio wataelewa
ReplyDeleteit is true, stop, stop, stop, killing our beloved once.God is watching you stop it.
ReplyDeleteUjumbe huo uandikwe kwa kiswahili ndiyo utawafikia walengwa ambao wengi hawajuwi ua hawafahamu hayo yaliyoandikwa.
ReplyDeleteMtoto mzuri Maashallah!
ReplyDeleteNa tunamuombea Mola ampe maisha marefu yeye na wenzake.
Ni ukatili usio na kifani hayo wanayofanya hao wapenda utajiri wa kijinga.
Mwenyezi Mungu atawalaani na kuwaadhibu hapa hapa duniani.
Tuungane sote kupinga ukatili huu.
MTOTO MZURI HUYO.
ReplyDeleteNi kweli kabisa, itumike lgha yetu ili woote waelewe maana sasa, tumeamua kuwalinda hawa ndugu zetu.
ReplyDeleteSo cute, bless her
ReplyDeleteTatitizo letu kubwa ni kuogopa Ukweli! Naona wengi hapa wanaogopa aibu hii ya kitaifa ya kuua watu wenye ugonjwa wa ngozi; Wantanzania tumezama sana katika ushebnzi wa kuamini uchawi! Hata wanaosema wamesoma au ni waamini wa madhehebu mbali mbali wengi bado wapo kwenye tamaduzi hizi za kishenzi: Makanisa, Misikiti na nyumaba za waganga wote wananufaika kwa mradi huu wa kishezi, yaani "uchawi". Makanisa na Misikiti wanahubiri zaidi juua ya kinga za Uchawi zaidi ya Neno la Quran Tukufu au Biblia takatifu. Tuanchane na Ushenzi. Tujiakwamue kwa kutoa Elimu mpya kwa watoto wetu.: Maana vijana wa leo na vizee vya juzi vyote vimezama kwenye Uchawi. Nyumba za watawa, Misikiti wote wamo humo kwenye ndimbwi la kuamini uchawi!
ReplyDeleteIts not Fair, Albino are not meant to spent the rest of their lives worrying or come up with a rescue plan to protect themselves. Their Meant to be productive in the society and pursue their goals and ambitions just like any other human being.
ReplyDeleteSasa hivi ukiandika Albino kwenye mtandao jina Tanzania linaibuka aibu aibu aibu
ReplyDeleteSIWAUWE 'ALBINO' (Sisitozo)
ReplyDeleteNatiririkwa machozi, naishiwa na maneno.
Kisa rangizo za ngozi, kama wazungu mfano,
Hadharani wazi wazi, mwawacharanga mikono,
La wote hili jukumu, siwauwe 'ALBINO'.
Imani zilowatoka, mwawawinda kwa mapanga,
Viungo vyao mwataka, kuvitolea muhanga,
Yenu taka kunyooka, acheni huo ni 'wanga'
La wote hili jukumu, siwauwe 'ALBINO'.
Siwauwe 'Albino', ulemavu si ugonjwa,
Si miguu si mikono, wala ngozi sijechanjwa,
Tuwaenzi kwa mifano, kwa uzima na ugonjwa,
La wote hili jukumu, siwauwe 'ALBINO'.
'Albino' tuwalinde, nao pia binadamu,
Huria nao warande, chochote siwahujumu,
Tuwe nao tuwapende, sote wana wa 'Adamu'
La wote hili jukumu, siwauwe 'ALBINO'.
Wenye imani potofu, mbali mzitokomeze,
Kutaka umaarufu, wao muwateketeze,
'Ilahi' hamumukhofu, kesho nini mmweleze?
La wote hili jukumu, siwauwe 'ALBINO'.
Acheni nao watambe, fani zote wapendeze,
Wenye vipaji waimbe, ma 'modo' wajitokeze,
"Msimu' kura waombe, na mote wajitokeze,
La wote hili jukumu, siwauwe 'ALBINO'.
Saba beti zinatosha, natowa msisitizo,
Wahukumiwe maisha, wenye haka ka mchezo,
Na adhabu zinotisha, hadi fika wafe nazo,
La wote hili jukumu, siwauwe 'ALBINO'.
HK
SWALI MOJA TU JANANI ..je Serikali hasa wizara ya afya mlishawahi kufikiria juu ya kupunguza au hata kufutilia mbali kodi kwenye lotion na mafuta ya kupunguza miale ya jua inayowatesa hawa watanzania?Kwa taarifa yenu nivea kutoka ujeruman yenye uwezo wa kupunguza makali ya miali ya jua kwenye ngozi kikopo kimoja si chini ya 60000 Tshs jamani hebu angalieni hili kwa umakini.
ReplyDeleteSomething should be done lazima Rais sasa hawa watu wanaofanya wenzao biashara tena Kwa kuwaua wanyongwe haraka iwezekanavyo. No excuse.
ReplyDeletekachuna jamani kazuri katoto...mungu awalinde
ReplyDeleteWatu wanafanya kampeni dhibi ya mauaji ya binadamu wenzetu, wengine wamekuja hapa na kampeni dhidi ya lugha. Suala hili linatakiwa kulaaniwa kwa lugha, kabila, dini, rangi zote bila ubaguzi, ili mradi mwishowe watato wetu waishi bila hofu
ReplyDeleteTafadhali serikali kuu hiingilie kati hili tatizo ikiwezekana lipelekwe jeshi la ulizi kabisa kwenye maeneo ambayo yamekua sugu. Hawa ni binadamu kama sisi wengine kwa nini wauawe kwa sababu ya ngozi yao. Atakayekamatwa anywenge ili iwe fundisho kwa wengine wenye mawazo potofu kama hayo.
ReplyDeleteNadhani imefika wakati Tanzania tuamue rasmi kuweka sheria ya kunyonga hadi kufa mtu yeyote atakayethibitika kuhusika na mauaji ya mlemavu wa ngozi.Hii iwahusu pia wanunuzi wa viungo vya binadamu.Vilevile iwe marufuku kupiga ramli,uganga wakienyeji,pamoja na watu kujiita madokta au maprofesa bila kusomea au kutunukiwa rasmi.China iliamua kuweka sheria kali za kunyonga,mbona ni marafiki zetu wa damu?KIGUGUMIZI KINATOKA WAPI?
ReplyDeleteMachozi yananitoka kila siku nikiona hizi taarifa, I wish kama ningekua milionea ningewajengea sehemu maalum na ulinzi wao, but why not tz government ?
ReplyDeleteYaani, inasikitisha sana. Ila Mungu ni mkubwa sana, sala za watu na machozi yetu hayaendi bure, Mungu ataonesha haki yake. Tuzidi kuwaombea ndugu zetu kwani nao hawakupenda kuwa hivyo walivyo.
ReplyDeleteMnapiga kelele bure kiingereza..kiswahili hao waganga wakienyeji lugha zote hizi hawazijui na wala hawana mitandao...mnacho takiwa kufanya nendeni vijijini huko mka toe darasa
ReplyDeleteMbona unatowa maagizo tu!! Wewe je?
DeleteWanunuzi wa viungo vya miili ya hawa albino ni viongozi wenyewe.
ReplyDeleteKwani tujiulize hivi serikali inashindwa kuweka mitego ya kuwakamata hawa wauwaji na wanunuzi kwa ujumla?
Wanaoua hata neno blog hawalijui maana yake!! Let's be more creative in finding better and more effective ways we can influence those that matter na sio wazungu unless ni janja ya kutafuta pesa ya mzungu na uhalali tu kutoka kwao! Just a thought!
ReplyDeleteWalengwa wa huu ujumbe ni nani???
ReplyDeleteWewe na mimi
DeleteMbona BBC waliweza kwenda mpaka huko na kujuwa ukweli na ninani hanahusika na kuonyesha jinsi waganga wanavyousika ktk mahuaji ya ndugu zetu.Lakin serikali himeshindwa kutega mitego na upelelezi kuwabaini hawa wahuwaji wa watoto?
ReplyDelete