Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva akizungumza wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Julius Malaba na kulia ni Kamishina wa Tume yaTaifa ya Uchaguzi,Prof. Amon Challigha
Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Siasa waliohudhulia Mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva (hayupo pichani) leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Francis Mutungi akichangia mada katika mkutano huo wa Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.
TUTAENDELEA KUPATA MAONI
KATIKA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA-JAJI LUBUVA
Na Chalila Kibuda.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema itaendelea
kupata maoni kwa wadau juu ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwa kutumia
mfumo mpya wa uchukuaji wa alama za
vidole kwa kutumia BVR ili kurahisisha wapiga kura.
Hayo ameyasema leo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC),Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa
na wadau wengine jijini Dar es Salaam ,Lubuva amesema mfumo wa uandikishaji wa
daftari la wapiga kura ni mpya hivyo ni lazima Tume itoe taarifa mara kwa mara na kupata mawazo mengine katika uboreshaji wa daftari hilo.
Lubuva amesema daftari la wapiga kura limekuwa na
malalamiko mengi kwa vyama vya siasa na kuona haja ya kubadili mfumo wa
uandikishaji kwa kuchukua alama za vidole kwa kutumia kifaa cha BVR ili kuondokana na malalamiko hayo.
“Tume inafanya kazi kwa kujitegemea hakuna mtu yeyote
anaweza kuipangia majukumu na hata mkutano wetu wa leo sio shinikizo la Mbunge
wa chama chochote kwani hii ni tume huru”amesma Jaji Lubuva.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi -CCM (Taifa) ,Nape
Nnauye amesema Tume imekuwa ikikaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa taarifa na
kuwa na shaka kutokana na masuala yaliyopo katika tume ni mazito ikiwemo
uboreshaji wa daftari la wapiga kura ambalo linatakiwa litumike katika kura ya
maoni pamoja na uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Amesema kama chama tawala wanataka kuona masuala haya
yanawekwa wazi na tume mara kwa mara ili wananchi wawe tayari katika
kuandikishwa katika daftari hilo .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...