Balozi wa Tanzania nchini Japan,Mhe. Salome Sijaona amepokea msaada wa magari mawili ya kubeba wagonjwa (Ambulance) na moja la zimamoto yaliyotolewa na mji wa Ibaraki, Japan kwa Serikali ya Tanzania ambao ni msaada kwa Tanzania katika kuboresha huduma za afya na kukabiliana na majanga ya moto.
Balozi wa Tanzania nchini Japan,Mh. Salome Sijaona akipokea mfano wa funguo kutoka kwa Meya wa Mji wa Ibaraki nchini Japan, Yasuhira Kimoto wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya magari hayo,yaliyotolewa kwa ajili ya kusaidia uboreshaji wa huduma ya afya na kukabiliana na majanga ya moto hapa nchini.
Sehemu ya magari hayo yaliyotolewa msaada kwa Tanzania.
Balozi Salome Sijaona akiwa katika Picha ya pamoja na kikosi cha jeshi la zimamoto la Mji wa Ibaraki,nchini Japan.
Balozi wa Tanzania nchini Japan,Mh. Salome Sijaona akimshukuru Meya wa Mji wa Ibaraki,Yasuhira Kimoto kwa msaada huo. Balozi aliwahakikishia wana Ibaraki msaada huo ni mchango mkubwa katika kuongeza kasi ya kuokoa maisha ya watu na mali zao hasa katika kipindi hiki ambapo miji inakua kwa kasi na idadi ya watu wanaohamia mijini ikiongezeka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...