Mkuu
wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Dani Makanga akizungumza na wajumbe kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waliofika ofsini kwake
kwa ajili ya kujitambulisha kabla ya kuendelea na ratiba yao ya mafunzo
kwa Vijana wa Halmashauri za Kasulu na Bihigwe leo mjini Kasulu.
Katikati ni Mkuu wa msafara huo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma
za Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi.
Esther Riwa na wa kwanza kushoto ni Afisa Vijana wa wizara hiyo Bi.
Amina Sanga.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Bw. Bernard Ntikabuze
(kushoto) akiagana na akipeana mkono na Afisa Vijana kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga wakati
walipotembelea ofisini kwa Mkurugenzi huyo leo. Katikati ni Mkuu wa
Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Bibi. Esther Riwa.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kasulu Bw. Muguha Titus Muguha akizungumza na
Vijana wanaoshiriki mafunzo kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (hawapo
pichani) yanayotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo. Kutoka kulia ni Afisa Vijana wa Wizara hiyo Bi.
Amina Sanga, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bibi. Esther Riwa,
Mkuu wa Kituo cha Maendeleo ya Vijana Sasanda kilichopo Mbeya Bw.
Laurian Massele na Afisa Vijana wa Mkoa wa Kigoma Bw. Edward Manase.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...