NA EXAUD MTEI
Wadau mbalimbali wa maswala ya usafirishaji,uchukuzi na watanzania kwa ujumla wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kusaidia kuchangia katika mkutano ulioandaliwa na CILT (the charted institute of logistics and transport) mkutano ambao unatarajiwa kufanyika kuanzia terehe 4 mwezi wa tatu hadi tarehe 6 katika hoteli ya mount meru mkoani Arusha.
Akizungumza na wanahabari mapema leo juu ya maandalizi ya mkutano huo wa kimataifa makamu mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo Bregedier HARISON JOSEPH MASEBO amesema kuwa mkutano huo utawakutanisha magwiji wa maswala ya usafirishaji na uchukuzi kutoka katika nchi mbalimbali barani Africa kwa lengo la kujadili maswala mbalimbali ambayo yanaikumba secta hiyo barani africa na Tanzania kwa ujumla.
Amesema kuwa mkutano huo ambao ni wa 12 kufanyika kimataifa umelenga kutafuta fursa mbalimbali za kutangaa biashara au bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na makampuni mbalimbali nchini,kutoa elimu kwa wadau kuhusu maswala mbalimbali ya usafirishaji pamoja pamoja na kutatua chanagamoto mbalimbali zinazokwamisha secta hiyo hapa nchini na barani Africa.
“tunawaomba wadau mbalimbali wajitokeze kwa wingi katika kuudhamini mkutano huu kwani ni nafasi pekee ya makampuni ya kitanzania kutangaza bidhaa zao kupitia mkutano huu kwa kuwa kutakuwa na watu kutoka maeneo mbalimbali Africa hivyo ni fursa pekee”alisema masebo
Baadhi ya mada ambazo zinatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano huo ni pamoja na ajali za barabarani na jinsi ya kukabiliaa nazo,usalama katika vyombo vya usafiri,kuibuka kwa dhana mpya katika logistic,msongamano katika bandari,msongamano wa magari barabarani,pamoja na mada nyingi ambazo zimetajwa kuwa ni manufaa kwa washiriki watakaoshiriki katika mkutano huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...