Mkurugenzi wa Muda wa Benki  ya NBC , Bw. Pius Tibazarwa akizungumza na wafanyakazi wa NBC katika warsha ya siku moja kuzungumzia maendeleo na mikakati ya benki hiyo kwa mwaka 2015. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi, ilijumuisha wakurugenzi wote wa benki hiyo, wakuu wa vitengo na mameneja wa matawi ya NBC nchi nzima.
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Hazina cha Benki ya NBC, Barton Hamisi,  akisisitiza jambo wakati wa warsha ya siku moja kuzungumzia maendeleo na mikakati ya benki hiyo kwa mwaka 2015. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi ilijumuisha wakurugenzi wote wa benki hiyo, wakuu wa vitengo na mameneja wa matawi ya NBC nchi nzima.
 Mkurugenzi wa Mauzo ya Reja Reja wa NBC ,Musa Jallow akimkabidhi cheti cha mtoa huduma bora wa mwaka 2014 Columba Kambi wa NBC Tawi la Dodoma katika hafla ya kupongeza wafanyakazi bora katika kitengo cha mauzo iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. 
 Wakuu wa vitengo mbalimbali vya Mauzo ya Reja Reja vya NBC Limited, wakimkabidhi tuzo Kemibaro Omuteku  (wa tatu kushoto) katika hafla ya kupongeza wafanyakazi bora katika kitengo cha mauzo iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...