Na Tinah Reuben, Globu ya Jamii
VIJANA sita waliokuwa katika mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanaodaiwa kupanga kuandamana mpaka kwa Rais Jakaya Kikwete kudai ajira,wamefikishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.
Wakisomewa mashtaka yao na mwendesha mashtaka wa serikali,Tumaini Kwema mbele ya Hakimu Mkazi ,Frank Mushi alidai kuwa,washtakiwa hao wanadaiwa kufanya fujo,kufanya mkusanyiko usiokuwa wa halali ili kuilazimisha serikali kuwapatia kazi na kushawishi kutenda makosa ya jinai kwa kuandamana mnamo Februari 15 mwaka huu eneo la Msimbazi Centre jijini Dar es salaam.
Washitakiwa hao ni George Gagris,Linus Immanuel,Pharas wera,Emmanuel Richard,Ridhwan Brayson na Jacob Joseph. Baada ya kusomewa mashtaka na mwendesha mashtaka,Tumaini Kwema,watuhumiwa hao wote kwa pamoja walikana mashtaka hayo.
Washtakiwa hao wamerudishwa tena rumande kutokana na kutokidhi masharti na vigezo vya dhamana,kesi hiyo itatajwa tena Machi 6 mwaka huu.
Baadhi ya vijana waliokuwa katika mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanaodaiwa kupanga kuandamana mpaka kwa Rais Jakaya Kikwete kudai ajira,wakiwa chini ya ulinzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,jijini Dar es salaam leo.
Watuhumiwa hao wakipandishwa kwenye gari ya polisi.
Picha na Emmanuel Massaka.
Picha na Emmanuel Massaka.
Swala la ajira ni vizuri tulielewe kama uwezo wa kupanua upatikanaji wa nafasi lakini hasa hasa ni uwezo wa kulipa mishahara. Ili tuweze kutengeneza ajira inabidi pato la nchi likiwemo pato la sekta binafsi likue. Hili si tatizo la Tanzania peke yake ni nchi nyingi zinahangaika. Uzuri wetu tuna ardhi, mvua ikinyesha tukalima hatufi njaa. Vijana ni vizuri muelewe dhana hii mtafute njia za kujikimu.
ReplyDelete