Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Mbenjamin Majoya (kushoto)akikabidhiwa msaada wa vifaa vya macho na Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambapo wanafunzi hao watapata huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.hafla hiyo ilifanyika katika hospitali ya wilaya ya mkuranga mkoa wa Pwani, wanao shuhudia ni Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dkt.Francis Mwanisi, Mratibu mradi Rebecca Kasika na Mratibu wa Taifa wa Huduma ya Macho Dkt.Nkundwe Mwakyusa(wapili kutoka kushoto)
Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo (kushoto)akimuonyehsa mashine ya kutengenezea miwani baada ya kukmkabidhi msaada wa sanduku la vifaa vya kupimia macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Mbenjamin Majoya kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambao watanufaika na huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.hafla hiyo ilifanyika katika hospitali ya Wilaya hiyo.kulia ni Mratibu huduma za macho mkuranga dkt.Gilbert Mrema.
Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo (kushoto) akijaribu kumpima miwani matroni wa Hospitali ya Mkuranga Rosemary Magombola wakati wa hafla ya kumkabidhi wa msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 kwa ajili ya kuwahudumia wanafunzi wa shule za msingi 122 za mkuranga ambao watanufaika na huduma hiyo ya upimaji macho pamoja na matibabu bure. Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Kaimu Mbenjamin Majoya (kulia) Mganga Mkuu wa Wilaya ya hiyo Dkt,Francis Mwanisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...