Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe Stephen Masatu Wasira amekutana na wadau wa sukari na kutoa tamko la serikali kuhusiana na kupanda kwa ya sukari hapa nchini.
Mhe Wasira amewaagiza wazalishaji na wafanya biashara wa sukari hapa nchini kuingiza sukari sokoni badala ya kuiweka kwenye maghala ili kushusha bei ya bidhaa hiyo muhimu
Agizo hili la waziri limekuja muda mfupi baada ya kupanda ghafla kwa bei ya sukari kutoka shilingi 1700/= iliyokuwa ikiuzwa awali hadi shilingi 3000 kwa kilo.
Aidha hali hiyo ilisababishwa na upungufu ulijiotokeza ghafla baada ya serikali kuthibiti uingizwaji holela wa sukari toka nje ya nchi.
Upande wa Wadau wameahidi kutoa ushirikiano kuhakikisha kuwa sukari inapatikana sokoni na kwa bei nafuu.
Alisema Serikali kwa kushirikiana na wadu wa sukari itaagiza tani 100000 ili kukabiliana na upungufu unaotokea kila mwaka wakati viwanda vinapofungwa kwa ukarabati.
“Serikali itatoa kibali cha kuingiza sukari tani 100000 mwezi machi ili kukabiliana na upungufu utakaojitokeza pindi ukarabati” alifahamisha Mhe Wasira.
Wazalishaji
na wafanyabiashara wa sukari wakimsikiliza kwa makini maamuzi ya serikali kuhusu bei ya sukari
Waziri
wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Stephen Wasira na Naibu wake (kushoto)
Mh.Godfrey Zambi, Bi. Sophia Kaduma Katibu Mkuu
(kulia) na Dkt.Yamungu Kayandabila (kushoto) wakifuatilia kwa makini
mjadala baina yao na wazalishaji na wafanyabiashara wa sukari katika mkutano
uliofanyika katika ukumbi wa Kilimo
Waziri
wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Stephen Wasira akisisitiza jambo wakati alipokutana na
wazalishaji na wafanyabiashara wa sukari hapa nchini katika ukumbi wa mikutano
hapa wizarani .
Waziri
wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Stephen Wasira akiendelea kuongea na wafanyabiashara wa sukari hapa nchini
TUNAOMBA PICHA YA PAMOJA YA BWANA WASIRA AKIWA AMESIMAMA NA WADAU WA SUKARI.
ReplyDeleteMdau wa mwanzo hapo juu sasa ukisikia 'ushari' ndio huo unaoutafuta. Hizo uzionazo hapo kwani hazitoshi?
ReplyDeletehahahahahahahahhaha
ReplyDeletehahahahaha nshajua unachotaka uone, kabadiri sio ile alovaa
ReplyDelete