Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe Stephen Masatu Wasira amekutana na wadau wa sukari na kutoa tamko la serikali kuhusiana na kupanda kwa ya sukari hapa nchini. Mhe Wasira amewaagiza wazalishaji na wafanya biashara wa sukari hapa nchini kuingiza sukari sokoni badala ya kuiweka kwenye maghala ili kushusha bei ya bidhaa hiyo muhimu 
 Agizo hili la waziri limekuja muda mfupi baada ya kupanda ghafla kwa bei ya sukari kutoka shilingi 1700/= iliyokuwa ikiuzwa awali hadi shilingi 3000 kwa kilo. 
 Aidha hali hiyo ilisababishwa na upungufu ulijiotokeza ghafla baada ya serikali kuthibiti uingizwaji holela wa sukari toka nje ya nchi.
 Upande wa Wadau wameahidi kutoa ushirikiano kuhakikisha kuwa sukari inapatikana sokoni na kwa bei nafuu. 
 Alisema Serikali kwa kushirikiana na wadu wa sukari itaagiza tani 100000 ili kukabiliana na upungufu unaotokea kila mwaka wakati viwanda vinapofungwa kwa ukarabati. 
 “Serikali itatoa kibali cha kuingiza sukari tani 100000 mwezi machi ili kukabiliana na upungufu utakaojitokeza pindi ukarabati” alifahamisha Mhe Wasira.
 Wazalishaji na wafanyabiashara wa sukari wakimsikiliza kwa makini maamuzi ya serikali  kuhusu bei ya sukari
 Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Stephen Wasira na Naibu wake (kushoto) Mh.Godfrey Zambi, Bi. Sophia Kaduma Katibu Mkuu  (kulia) na Dkt.Yamungu Kayandabila (kushoto) wakifuatilia kwa makini mjadala baina yao na wazalishaji na wafanyabiashara wa sukari katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Kilimo 
 Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Stephen Wasira  akisisitiza jambo wakati alipokutana na wazalishaji na wafanyabiashara wa sukari hapa nchini katika ukumbi wa mikutano hapa wizarani .
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Stephen Wasira akiendelea kuongea na wafanyabiashara wa sukari hapa nchini 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. TUNAOMBA PICHA YA PAMOJA YA BWANA WASIRA AKIWA AMESIMAMA NA WADAU WA SUKARI.

    ReplyDelete
  2. Mdau wa mwanzo hapo juu sasa ukisikia 'ushari' ndio huo unaoutafuta. Hizo uzionazo hapo kwani hazitoshi?

    ReplyDelete
  3. hahahahahahahahhaha

    ReplyDelete
  4. hahahahaha nshajua unachotaka uone, kabadiri sio ile alovaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...