Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu mapambano ya kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino),Said Ndonge akiwa na wajumbe wa kamati hiyo, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maandamano wanayotarajia kuyafanya Machi 3 Mwaka huu jijini Dar es Salaam. (Picha Emmanuel Massaka).
NA Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii.

Kamati ya kuratibu mapambano ya kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)umepingana na kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ulemavu Ngozi Taifa, Bw. Ernest Kimaya kuwa kamati iliyoandaa matembezi ya hisani ni ya watu wahuni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw, Said Ndonge amesema kauli ya mwenyekiti wa Taifa  ni ya ubaguzi na inatoa nafasi ya adui kuendelea kwa mauaji ya jamii yetu.

Amesema tangu mwaka 2006  waliouwawa ni 76 na 15 kubaki na ulemavu wa kudumu "Hivyo sisi wanaharakati wa kupambana na kukomesha udhalimu huu tunaendelea kulaani vitendo wanavyotutendea baadhi ya jamii yenye imani potofu za kishirikina.

Kamati hiyo imesema haiutambi umoja wa chama cha AlbinoTanzania kutokana na viongozi wake kushindwa kusimamia majukumu yake na badala yake kutaka kuleta mfumo wa kubaguana na kumfanya adui apate nafasi kutushambulia. 
Hata hivyo, Bw. Ndonge amesema maandamano yako palepale kutokana na Jeshi la Polisi kutoa ulinzi kwa siku ya maandamano  yanayotarajiwa kufanyika Machi 2 mwaka huu.
Kamati hiyo imetaka wadhili wajitokeze kufadhili maandamano hayo katika kuokoa watu wenye ulemavu wa ngozi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...