Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akizungumza na mwanamuziki mkongwe wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA wakati mwanamuziki huyo alipokutana na Waziri huyo jijini Washington DC katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, na kwa upande wa Mwana FA yupo nchini Marekani kwa ajili ya matembezi yake binafsi hata hivyo alienda ubalozini hapo kwa ajili ya kumsalimia Balozi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja na mwanamuziki mkongwe wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA wakati mwanamuziki huyo alipokutana na Waziri huyo jijini Washington DC katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, na kwa upande wa Mwana FA yupo nchini Marekani kwa ajili ya matembezi yake binafsi hata hivyo alienda ubalozini hapo kwa ajili ya kumsalimia Balozi. Kulia ni rafiki wa mwanamuziki huyo ambaye pia ni mfanyabiashara, Swalah Saidi. Picha zote na FelixMwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongereni sana, hii inaonyesha uhusiano mzuri alionao Balozi wetu na Watanzania wenzake.

    Namkumbuka alipokuwa Canada mama huyu akitutumia fedha za kusherehekea mwaka mpya (sikumbuki vizuri)sisi wanafunzi tuliokuwepo Chuoni kipindi kile.

    Of course tulikuwa wanafunzi wachache tu siyo kama sasa hivi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...