Mkurugezi wa Kundi hilo Mkubwa Fella kwanza alianza kwa kutoa shukran zake kwa Mwenyezi Mungu, Mashabiki, Wadu na vyombo vyote vya habari kwa kuweza kutoa sapoti kwa vijana hao tangu walipo toa Kazi yao ya kwanza kabisa mpaka kufikia Leo wamepata mualiko mkubwa kabisa wa kwenda kufanya show UK.
Kwa upande wa Msemaji mkuu na Kiongozi wa Band Aslay Isihaka amesema kuwa wanafuraha sana kwa kupata mualiko huo lakini pia wanashukuru kwa mungu, mashabiki na wale wote wanaonyesha sapoti katika muziki wao. Aslay amesema   kuwa watakwenda kufanya Kazi nzuri huko ili kuleta sifa ya muziki wa hapa nyumbani na hata heshima ya Taifa kwa ujumla.Kwa upande mwingine Vijana hao Wametoa shukrani zao kwa Viongozi wao Mkubwa Fella, Bab Tale, Chambuso, Mh Temba na Shirko kwa usimamizi Mzuri wa Kazi hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...