Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa(katikati)akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni (hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya JayMillions,Wengine katika picha kushoto ni Balozi wa Promosheni hiyo Hilary Daud”Zembwela” na kulia ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Uwezo Magendege, 22, ni mshindi wa kwanza wa zawadi nono ya siku ya pesa taslimu Sh. 100m/- za promosheni iliyozinduliwa siku 19 zilizopita na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.
Hadi kufikia leo ni Sh. 126m/- pekee zilizokwisha kuchukuliwa na Uwezo, washindi wengine wawili – Hyness Petro Kanumba from Rukwa and James Mangu (Mwanza) – wa Sh. 10m/- na sita – Chiliphod Wanjala (Mwanza), Janeth Ngannyange (Njombe), Evarista A (Mwanza), Stanley Bagashe (Shinyanga), Ramadhani H. Maulid (Dodoma) and Lucas M (Shinyanga) – wa Sh. 1m/-. Kiasi cha zaidi ya Sh. 5bn/- (ambazo ni sawasawa na magari madogo 428 ya muundo wa mgongo wa kobe) zingeweza kunyakuliwa na wateja iwapo wangetuma neno “JAY” kwenda 15544 kucheki kama wameshinda.
Uwezo ni mkazi wa wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa. Mnamo Alhamis Januari 29, 2015, Uwezo alipokea simu ambayo ilipelekea maisha yake kubadilika milele alipotaarifiwa kuwa amejishindia Sh. 100m/- kutoka katika mamilioni ya shilingi yanayogawiwa kupitia promosheni ya JayMillions ya Vodacom Tanzania kwa siku hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...