Baadhi ya bidhaa zilizoteketezwa na Maofisa wakaguzi wa TFDA wilayani Sikonge.
Maofisa wakaguzi wa TFDA kanda ya kati wakijiandaa kuteketeza bidhaa zilizoisha mda wake ikiwemo vinywaji wilayani Sikonge (picha na Allan Ntana).
Na Allan Ntana, Sikonge
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati imefanikiwa kukamata na kuteketeza bidhaa mbalimbali za chakula, vinywaji, dawa za binadamu na mifugo, vipodozi na vifaa tiba vilivyoisha muda wake na vingine feki vyenye thamani ya zaidi ya sh mil.5 katika halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
Akisoma taarifa ya ukaguzi mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo hapo juzi Afisa Mkaguzi wa Chakula Kanda ya Kati Sifa Chamgenzi alisema ukaguzi huo ulilenga kuangalia ubora na usalama wa dawa za binadamu na mifugo, uwepo wa vipodozi vilivyopigwa marufuku na bidhaa zingine zilizoisha muda wake wa matumizi.
Alisema lengo la TFDA ni kufuatilia utekelezaji wa sheria na.1 ya mwaka 2003 ya chakula, dawa na vipodozi kwa wauzaji na wasindikaji wa vyakula na dawa na kuongeza kuwa zoezi hili lililenga kutekeleza mpango kazi wa Mamlaka hiyo wa kufuatilia ubora na usalama wa bidhaa hizo kwa mtumiaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...