Naibu waziri wa maji Amos Makalla amefanya ziara ya kikazi wilayani Hanang leo kwa kutembelea mradi wa maji kijiji cha Ishponga na kuagiza Generator lifungwe haraka kurejesha huduma ya maji iliyosimama kwa miezi mitatu
Amekagua mradi maji Kateshi na kuhaidi kushughulikia tatizo la nishati ya umeme linalopelekea mamlaka kushindwa kumudu gharama za uendeshaji
Ameweka jiwe la msingi mradi mkubwa wa maji kijiji cha Simbay kata na tarafa ya Simbay
Aidha ameagiza mradi wa mradi wa maji wa Endasak utakaohudumia vijiji vitatu wiki ijayo halmashauri itangaze zabuni za kumpata mkandarasi kwani tayari wizara imeshatuma shilingi milioni 300
Ameagiza watu 39 waliovamia chanzo cha maji Endasak wapewe notisi waondoke eneo la chanzo
Naibu waziri wa maji Mhe. Amos Makalla akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye huko Hanang leo
Naibu waziri maji Amos makalla akiweka jiwe la msingi mradi maji kijiji cha Simbay- Hanang
Naibu waziri maji kushoto na mbunge wa Hanang wakiwasikiliza viongozi wa kijiji cha Ishponga
Naibu waziri Amos Makalla akizungumza na mbunge wa Hanang na waziri ofisi ya Rais (Mahusiano) Dr Mary Nagu
![]() |
Naibu waziri maji akikagua tanki la maji mji wa Katesh |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...