WADAU 100
waliofanikisha kwa namna mbalimbali katika kipindi cha miaka 15 tangu kuanzishwa
Tamasha la Pasaka nchini wanatarajiwa kupewa tuzo wakati wa tamasha la mwaka
huu.
Taarifa kwa
vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya
tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa wadau hao ni wanasiasa, viongozi wa
dini, wafanyabiashara na waandishi wa habari.
“Wapo wengi
waliotusaidia kufikia hapa tulipo, lakini tumeteua 100 hawa watapokea kwa niaba
ya wengine, ikiwa ni shukrani kwa kutusaidia kwa namna mbalimbali.
“Wapo
waliotusaidia wanatoka Dar es Salaam na wengine mikoani, hivyo wale wa mikoani
tutawapa tuzo zao wakati tukienda katika matamasha ya huko na wale wa Dar es
Salaam watapokea siku yenyewe ya Pasaka,” alisema Msama.
Alieleza
kuwa si kazi rahisi kuweza kusimamisha tamasha kubwa kama hilo kwa miaka 15,
pia si kazi ya yeye peke yake bali ni ushirikiano wa watu mbalimbali ambao anaona
kuna umuhimu wa kuwashukuru.
Alisema
watawapa tuzo maalum pamoja na vyeti ambavyo anaamini kwa kiasi fulani vinaweza
kuwafanya wahisi kweli mchango wao umetambuliwa.
Mwaka huu
Tamasha la Pasaka linatimiza miaka 15 tangu lianzishwe, ambapo waandaaji
wamepanga tamasha kubwa la kuendena na sherehe hizo.
Tayari
wasanii maarufu kutoka nje ya Tanzania wameshathibitisha kushiriki wakiwemo Rebecca Malope na Solly Mahlangu ‘Obrigado’ wote kutoka AAfrika
Kusini na raia wa Uingereza Ifeanyi Kelechi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...