DSC_0081
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (aliyefunikwa mwamvuli) akiwasili kwenye sherehe ya siku ya wanawake duniani iliyoandaliwa na Zanzibalicious Women Group na kufanyika ndani ya ukumbi wa Salama, Bwawani Hotel mwishoni mwa wiki.

Na Mwandishi wetu, Zanzibar
UTAFITI uliofanywa na taasisi ya wanawake nchini Zanzibar ya Zanzibalicious Women umeonyesha kuwa asilimia 40 ya wanawake Zanzibar, wanaishi katika mazingira duni ya umasikini kwa kutojitambua na kukosa elimu ya uelewa jinsi ya kukabiliana na mazingira waliyomo.

Akisoma risala siku ya wanawake mbele ya mgeni rasmi mke wa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mama Mwanamwema Shein , katika siku ya wanawake hafla iliyofanyika hoteli ya Bwawani, Mweka hazina wa Zanzibalicious Women Group, Shekha Hilal alisema hali hiyo ni changamoto kubwa na sasa kunatafutwa namna ya kumfikia mwanamke huyu ambaye ameshagota katika jamii yetu.

“Mama Shein asilimia hii ni kubwa saana, na sisi kama wanawake ambao tayari tumejaaliwa elimu na tunajitambua, ikiwa ni pamoja na tayari tumepiga hatua kimaendeleo katika nyanja mbalimbali, tumeguswa sana sana na suala hili.” Alisema Shekha.

Zanzibalicious ni umoja wa wanawake wanaoishi Zanzibar,ulioanzishwa mwaka 2011,na kusajiliwa rasmi mwaka 2013, ikiambatana na uzinduzi uliofanyika tarehe 28 Machi 2014.
DSC_0227
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein akiwasili kwenye sherehe ya siku ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na Zanzibalicous Women Group mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Salama, Bwawani Hotel.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nyie wenyewe hamjitambui msingekwenda vichwa wazi!

    ReplyDelete
  2. Wanawake ni muhimu sana katika jamii, wakielimika wakaendelea jamii nayo inakuwa imehamasika na kuendelea. Hivyo wanawake hawa wawezeshwe kujikwamua kutokana na maisha hayo duni. Wakina mama wanaweza wakiwezeshwa

    ReplyDelete
  3. Nadhani wanaweza au wangekwishafika mbali kimaendeleo, binafsi nadhani ni ile dhana iliyokuwepo tangu zama hizo kuwa mwanamke siku zote ni mtu wa 'stara' ambae iliaminika si mtu wa kukuru kakara mithli ya mwanamme. Hali hii au background hii imepelekea wanawake wengi kuridhika na maisha yao ya kila siku ambayo wengi wao yapo katika hali duni, kama kuendelea utakuta ni wachache sana nao pengine kwa mujibu wa nafasi zao ama uwezo wao wa kimaisha na upeo wa kuweza kwenda na wakati kulingana na maisha tuliyonayo katika kizazi hiki cha leo. Ni jitihada za dhati zikifanyika katika kuwaelimisha, kuwaongoza na kuwawezesha wanawake hao, naamini hali hiyo duni inayowakabili itaweza kutoweka,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...