Baada ya Mji wa Ibaraki kutoa magari mawili ya kubeba wagonjwa na moja la huduma ya zimamoto mwezi Februari, 2015, Miji mingine ya Japan nayo imeunga mkono jitihada hizo.
Pichani Mhe. Salome Sijaona, Balozi wa Tanzania Japan na Mhe. Toshima Suzuki, Meya wa Mji wa Tochigi wakionyesha mkataba wa makubaliano wa msaada wa magari 10 ya huduma, gari 6 ni kwa ajili ya Zimamoto na 4 kubeba Wagonjwa. Gari mbili (moja la wagonjwa na moja la huduma ya zimamoto) zimetolewa Machi 24 na mji huo kwa mwaka 2015 na gari nyingine 8 kwa kipindi cha mwaka 2016/17.

Vile vile Mjiwa wa Hakusan - Ishikawa Prefecture umetoa gari mbili za huduma ya Zimamoto Machi 25, 2015 na kuahidi kuendelea kufanya hivyo kwa mwaka ujao wa fedha.
Kulia ni Afisa wa Ubalozi, Bw. Francis Mossongo, akipokea Nozzle ya gari ya zimamoto kutoka kwa Bw. Noriaki Yamada, Meya wa Mji wa Hakusan kama ishara ya kupokea gari hizo.
Picha ya Gari zilizopokelewa kutoka kikosi cha zimamoto cha mji wa Kanazawa. Gari hizo zitakabidhiwa kwa kikosi cha Zimamoto Tanzania.
Vile Vile Ubalozi umeshizikiana na Hakusan Chamber of Commerce ya mji wa Hakusan kuanzisha aina mpya ya kahawa kwa jina la Hakusan-Kilimanjaro Coffee. Lengo ni kuunganisha na kutangaza mlima ya Kilimanjaro na Mlima Hakusani. Chini ni picha ya Kahawa hiyo. Kila kikombe kimoja kinachouzwa kiasi cha Yen 10 (sawa na Tsh. 150) inatumika kwa ajili ya kulinda mazingira ya milima hiyo miwili ikiwa ni pamoja na kupanda miti.

Juu ni mfano wa kahawa hiyo ikiwa kwenye vifungashio viwili tofauti.

Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania Japan
26. Machi 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...