Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akilifunguwa Kongamano la Wanawake na Uongozi katika Katiba inayopendekezwa lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi akitoa nena la shukrani kwa Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kulifungua Kongamano la Wanawake na Uongozi.
Mtangazaji wa Zamani wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni Zanzibar Karume House Bibi Neema Mussa Maisara akiipitia Katiba iliyopendekezwa kwenye Kongamano la Wanawake na Uongozi hapo Grand Palace Malingi Mjini Zanzibar. Kulia yake ni msanii maarufu Zanzibar Bi Tele, Naibu Katibu Mkuu wa Wazazi Zanzibar Bibi Salama Aboud Talib na Makamu mwenyekiti Mstaafu wa UWT Zanzibar Bibi Mvita Mussa Kibendera.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...