Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban ki Moon, akihutubia wakati wa uzinduzi wa  ripoti mpya  kuhusu mkakati wa kimataifa kuhusu vuguvugu la  kila  mwananamke, kile mtoto, ( every woman, every child) mkakati ambao aliuratibu mwaka 2010 .
Na Mwandishi Maalum.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban ki Moon,  amesema kama si utashi wa kisiasa,  kujituma, na kujitolea kulikofanywa na  viongozi mbalimbali aliowaomba kufanya naye kazi kwa karibu huku wengine wakijitolea wenyewe,  uhai wa  wanawake na watoto  2.4 milioni  usingeokolewa.
Ban Ki Moon ameyasema hayo siku ya  Jummane wakati wa uzinduzi wa  ripoti mpya  kuhusu mkakati wa kimataifa kuhusu vuguvugu la  kila  mwananamke, kile mtoto, ( every woman, every child) mkakati ambao Ban Ki Moon  aliuratibu mwaka 2010 .
“ Siri kubwa ya mafanikio ya  mkakati huu ni  uwajibikaji.  Nilipoanzisha mkakati huu niliwaomba baadhi ya viongozi wanisaidie, wapo waliosaidia katika uhamasishaji wa  raslimali fedha,  wapo kama Rais Jakaya  Kikwete wa Tanzania na waziri Mkuu wa Canada ambao walisimamia suala zima la  habari  na uwajibikaji,  mchango wao, kujituma kwao na uthubutu wao ndiyo umetufikisha hapa , tumeweza kuokoa maisha ya wanawake  na watoto wengi na kazi bado inaendelea” ameeleza  Katibu Mkuu
Akasema   mkakati huo aliouzisha   wa  kila mwanamke, kila mtoto  na ambao chimbuko lake ni lengo namba  nne na tano la maendeleo  ya millennia  ni  mkakati ambao si tu   umekuwa wa mafanikio makubwa lakini umegusa  hisia za wadau mbalimbali za watu wengi .
Malengo namba nne na  tano ya maendeleo ya millennia na ambayo yanafikia ukingoni  mwisho mwa  mwaka huu  yanajikita katika kupunguza idaidi ya vifo vya wanawake na idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
“Nilianzisha mkakati huu kwa sababu mimi mwenyewe nimeguswa katika maisha yangu utoto wangu kwa kuondokewa( kufariki) kwa kaka na dada zangu kwa matatizo ambayo yangeweza kuzuilika.  Simulizi  alizokuwa akisimuliwa na mama yake   juu  hofu kuu wanayokuwa nayo wanawake wanapokwenda kujifungua vile vile ni moja ya hamasa iliyonifanya nianzishe mkakati huu.  Lakini pia katika utekelezaji wa majukumu yangu nimekutana na visa vingi vilivyoongea  nia  na ari   kuwa na mkakati huu” ameeleza Ban Ki Moon
Ripoti hiyo ambayo uzinduzi wake umekwenda sambamba na mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu hadhi ya wanawake,  inabainisha kwa kina mafanikio na changamoto mbalimbali za utekelezaji wa  katika eneo hilo linalohusu afya ya mama na mtoto.
Ban Ki Moon amesema amefarijika na kutiwa moyo sana
Kwa mfano Makati huo ambao umegusa hisia wa wadu  mbalimali wakiwamo  viongozi wakuu wan chi na serikali,  asasi zisizo za kiraia, wanaharakati  na  makampuni binafsi.
Ban ki Moon amesema ushirikiano wa karibu baina yake na Viongozi wakuu wa mataifa mbalimbali umesaidia kuokoa maelfu ya maisha ya wanawake ambao wangepoteza maisha yao wakati wa kujifungua.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban ki Moon, akiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika moja ya mikutano ya kupanga mikakati kuokoa mama na mtoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...