MRATIBU WA KIBIKI CUP HARUNA SALEH AKIWA NA MDAU WA SOKA FRANK KIBIKI
MRATIBU WA KIBIKI CUP HARUNA SALEH AKIWA NA MDAU WA SOKA FRANK KIBIKI na wanahabari
---------------------------------
LIGI inayoshirikisha watoto
walio chini ya umri wa miaka 16, inaloitwa Iringa Kibiki Childrens Cup
2015 yenye lengo la kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino) inatarajia
kuanza kutimua vumbi jumamosi ikishirikisha timu nane za manispaa ya Iringa.
Mratibu wa ligi hiyo, Haruna Salehe
alisema lengo la mpira huo ni kukuza vipaji vya watoto na kueneza ujumbe wa
kupinga ukatili na mauaji yanayofanywa kwa walemavu wa ngozi nchini.
Alisema ligi hiyo iliyobuniwa na
kuendeshwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru, inatarajia kushirikisha
timu nane za watoto katika manispaa ya Iringa.
“Lengo kubwa ni kukuza vipaji na
kueneza ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa wenzetu walemavu wa
ngozi ambao wamekuwa wakiuawa kila siku bila huruma jambo ambalo, hatutaki
liendelee kwenye jamii yetu,”alisema
Alisema michuano hiyo itakuwa
ikifanyika katika uwanja wa mwembetogwa ambao ni wa wazi ili watu wengi wapate
nafasi ya kushiriki.
Kwa upande wake, mdau wa soka na
mwanahabari Frank Kibiki alisema ameamua kubuni ligi hiyo ili
kupanda mbegu ya kupenda michezo na kutambua vipaji vya soka tangu utotoni, ili
iwe rahisi kuwapata wachezaji bora siku zijzo.
“Mpira ni ajira na huu hauna dini,
kabira wala rangi, watu wote hata watoto wanaweza kushiriki kwenye mpira hivyo
tumebuni jambo hili ili kuendelea kukuza vipaji huku tukibeba ujumbe wa kupinga
ukatili kwa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi,”alisema
Kibiki ametoa wito kwa wadau
mbalimbali wa soka kushiriki kwenye michuano hiyo ili kusaidia kuibua vipaji na
kulifanya soka la Iringa kuwa endelevu.
Alisema tayari shirikisho la Soka,
manispaa ya Iringa wametoa Baraka za kuanza kwa ligi hilo, ambalo watoto
wameshaewa mafunzo ya kuwa waamuzi na washika vibendera hiyo wao wenyewe
watajiongoza.
Kwa upande wao wadau wa soka,
manispaa yaa Iringa waliitaka serika kutambua mchango na kuwekeza kwenye soka
ili kusaidia kupandisha timu zilizopo na kuendelea kuibu vipaji ikiwemo
michuano ya watoto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...