JE UNA MALALAMIKO JUU YA BILI YAKO YA MAJI YA KILA MWEZI, UNA DENI SUGU LA DAWASCO, UNA TAARIFA ZA WATU WANAOHUJUMU MIUNDO MBINU YA MAJI, UNAHITAJI KUUNGANISHIWA HUDUMA YA MAJI NYUMBANI KWAKO SHIRIKA LA MAJI SAFI NA MAJITAKA DAR-ES-SALAAM (DAWASCO) LINAKUKARIBISHA MTEJA, MWANANCHI, TAASISI NA MASHIRIKA KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI YANAYOANZA RASMI TAREHE 16 HADI 22 MACHI 2015 NCHINI KOTE YENYE KAULI MBIU YA “MAJI KWA MAENDELEO ENDELEVU”

KATIKA KUADHIMISHA WIKI YA MAJI DAWASCO KAMA MTOA HUDUMA MKUU WA HUDUMA YA MAJISAFI NA MAJITAKA JIJINI DAR ES SALAAM IMEANDAA DAWATI MAALUM KWA WATEJA WAKE NA WANANCHI KWA UJUMLA KATIKA SEHEMU KUU TATU: DAWASCO KINONDONI (ILIYOPO NYUMA YA JENGO LA AIRTEL), DAWASCO MAKAO MAKUU (BARABARA YA SOKOINE DRIVE), NA DAWASCO BOKO.

MADAWATI HAYA YATATUMIKA KUJIBU MASWALI NA KUTOA UFUMBUZI WA MATATIZO YA WANANCHI WANAOHUDUMIWA NA DAWASCO, KUTOA ELIMU JUU YA HUDUMA ZA MAJI ZITOLEWAZO NA DAWASCO, KUONGEZA UELEWA JUU YA SERA YA MAJI, KANUNI, MIONGOZO, ULINZI WA MIUNDOMBINU YA MAJI NA MATUMIZI SAHIHI YA DIRA ZA MAJI n.k MADAWATI HAYA YATAKUWA WAZI WIKI NZIMA KUANZIA TAREHE 16 HADI 22 MACHI KUANZIA SAA 2:00 ASUBUHI HADI SAA 12:00 JIONI KILA SIKU.

KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU HUDUMA KWA WATEJA 022 2194800 NA 0658-198889
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...