Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam limetoa misaada ya kibinadamu kwa watoto yatima wa kituo cha Msimbazi centre ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Maji yaliyoanza mapema tarehe 16 na kufika kilele 22 machi mwaka huu.

Akiongea na vyombo vya habari, Afisa Uhusiano wa DAWASCO, Bi Everlasting Lyaro alisema msaada huu ni sehemu ya jamii wanayotoa huduma hiyo kila siku.

“sisi kama DAWASCO tumeguswa na mahitaji ya watoto hawa na kama sehemu ya Jamii na katika kuadhimisha wiki ya Maji tumeona tutoe msaada wa hali na mali kwa watoto hawa ili kuwakumbusha jamii umuhimu wa kukumbuka jamii kama hizi” alisema Lyaro

Nae mlezi wa watoto hao sister Anna Francis alishukuru kwa msaada huo na kuitaka jamii kukumbuka watu wenye mahitaji mbalimbali kama sehemu ya ibada na utu katika sehemu ya maisha ya binadamu.

Maadhimisho ya wiki ya Maji yalianza mapema wiki iliyopita na yalifika kilele Jumapili hii ambako kitaifa yalifanyika mkoani Musoma.
Ofisa Uhusiano DAWASCO, Everlasting Lyaro (kushoto) akikabidhi msaada wa chakula kwa mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Msimbazi Opharn Centre, sista Anna Francis katika kuhitimisha wiki ya Maji kwa kutoa msaada kwa jamii inayowazunguka jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...