Mkazi wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya Edward Mbugi,amekabidhiwa fedha zake kiasi cha shilingi Milioni 1/-na Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Nyandaya Kusini,Macfadyne Minja,alizojishindia kupitia promosheni ya Jay Millions inayoendeshwa na kampuni hiyo. 
Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa fedha zake za Ushindi, mshindi wa Shilingi Milioni 1 wa Promosheni hiyo, Edward Mbugi, amesema kwanza kabisa hakuamini kama ameshinda kwani kumekuwa na kasumba ya washindi wengi wanaoshinda kupitia promosheni kama hizi zinazoendeshwa na kampuni za simu lazima ni wakazi wa Jijini Dar es Salaam tu. 
Ila nimefurahishwa sana na promosheni hii ya Jay Millions ni yakipekee inatoa washindi kila kona ya nchi.
Napenda kuwaomba Watanzania kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Vodacom Tanzania nchini katika kujenga na kuimarisha maisha ya Watanzania na kuwa murua zaidi. 
"Promosheni ya Jaymillions naona inalenga kuwakomboa kimaisha watanzania hususani wenye kipato cha chini hasa wajasiriamali wadogo wadogo kama vile; wamachinga, mama ntilie, ambapo kwa kiasi kikubwa tunajua watu wa aina hii wanahitaji msaada ili kujiendeleza kiuchumi. 
Kwa fedha ambazo baadhi ya washindi tayari wamezipata wengi zimewasaidia kujikwamua na kujiendeleza kimaisha," alisema Mbugi.
 Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Nyasa, Macfadyne Minja (kushoto) akipokea pesa kiasi cha shilingi Milioni 1/- toka kwa wakala wa M-PESA jijini Mbeya kwa ajili ya kumkabidhi rasmi mkazi wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya, Edward Mbugi (kulia) alizojishindia kupitia promosheni ya JayMillions wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini humo hivi karibuni. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay au AUTOkwenda 15544.
 Mkazi wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya, Edward Mbugi (kushoto) akipokea pesa kiasi cha shilingi Milioni 1/-kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Nyasa, Macfadyne Minja, alizojishindia kupitia promosheni ya JayMillions wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini humo hivi karibuni. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay au AUTO kwenda 15544.
 Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Nyasa, Macfadyne Minja (kulia) na Meneja wa Vodashop Baraka Musabila (kushoto) wakimshuhudia Edward Mbugi, ambaye ni Mkazi wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya akionesha kitita chake cha shilingi Milioni 1/- alizojishindia kupitia promosheni ya JayMillions inayondeshwa na Vodacom Tanzania,wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini humo hivi karibuni. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay au AUTO kwenda 15544.
Mshindi wa shilingi Milioni 1/- mkazi wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya, Edward Mbugi, kupitia promosheni ya JayMillions inayondeshwa na Vodacom Tanzania, akizihebu pesa zake baada ya kukabidhiwa rasmi  na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Nyasa, Macfadyne Minja (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Mbeya hivi karibuni. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay au AUTO kwenda15544.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...