
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya Tehama, Al Amin Yusuph akiwasilisha mrejesho wa kazi ya kikundi chake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.(Picha na zote Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi Wetu
WAKAZI wa kijiji cha Ololosokwan wamesema kwamba ujio wa kijiji cha digitali katika kijiji chao ni neema kwao kwani kitawasaidia kukabiliana na changamoto kubwa za maisha zinazowakabili.
Kauli hiyo wameitoa mwishoni mwa wiki wakati wa kuhitimisha warsha ya siku saba ya kuangalia fursa na changamoto zitakazoambatana na mradi huo wa miaka mitatu unaodhaminiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kwa kushirikiana na kampuni ya Ki-elektroniki ya Samsung.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake waliohudhuria warsha hiyo ambapo wataalamu mbalimbali wanaohusika na mradi huo walikutana kujadili changamoto na namna ya kukabiliana nazo, Salangat Mako, alisema kwamba tatizo la miundombinu, Afya na Elimu wanaamini litakabiliwa na mradi huo.
Alisema kuna shida kubwa ya elimu kutokana na mazingira yaliyopo ambapo wanafunzi wanalazimika kutembea kilomita 14 kwenda na kurudi shule hali inayodhoofisha ari ya kujifunza.

Mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya elimu kutoka UNESCO, Jennifer Kotta akitoa mrejesho wa kilichojadiliwa na kikundi chake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...