UONGOZI  wa Simba umemtangaza mwandishi wa habari wa siku nyingi,Haji Sunday Manara kuwa msemaji mpya wa klabu hiyo ya wekundu wa Msimbazi.

Katibu mkuu wa Simba Steven Ally ameiambia Globu ya Jamii kuwa Manara atachua nafasi ya Humphrey Nyasio ambaye atapangiwa majukumu mengine.

"Kamati ya Utendaji ya Simba  imemkabidhi jukumu Manara baada ya kujiridhisha pasi na shaka uzoefu wake katika masuala ya michezo na pia uzoefu wake katika mambo mbalimbali ya kiutawala, hivyo kuwa na imani kwamba ataifanya kazi yake  vizuri  kama walivyofanya watangulizi wake."alisema Ally.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. MsemaKweliMarch 18, 2015

    Hongera Haji!!! Sasa piga kazi usifanye yale mambo ulipokuwa diwani. Mdogo wako Sakina yupo wapi siku hizi?

    ReplyDelete
  2. Mchizi wangu wa Bunge huyu 7A poa sana kaka piga kazi!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...