WAZIRI wa Maliasili na Utalii Lazaro, Nyalandu leo amepokea ndege aina ya Micro Light Nyinja 5H-HEL, kutoka kwa kampuni inayojihusisha na masuala ya utalii ya Tanganyika Wildlife Safari itakayosaidia harakati za kukomesha masuala ya uuaji wanyama pori na ujangili.

Akipokea ndege hiyo jijini Dar es Salaam,Waziri Nyalandu alisema ndege hiyo ni mpya kabisa na ya usalama wa hali ya juu kutokana na muunekano wake kuwa wakisasa zaidi.

"Hii ndege ni salama zaidi kwasababu yenyewe imejengwa na parachuti yake endapo kunatokea chochote wakati ikiwa angani inafunguwa parachuti ambayo itaisaidia yenyewe pamoja na watu waliomo hivyo ni ya uhakika zaidi". alisema Nyalandu.

Nae Mwenyekiti wa kampuni iliyotoa ndege hiyo ya Tanganyika Wildlife Safari, Eric Pasanisi, alisema ndege hiyo inathamani ya Dola laki mbili na ishirini elfu ($220,000), na kueleza sifa mbalimbali za ndege hiyo.

"Ndege hii ni ndege yenye spidi ndogo zaidi kuliko ndege yeyote, kwani mwendo wa ndege hii ni karibu sawa na mwendo wa gari tu, kutokana na hali hiyo itakuwa rahisi zaidi kuwabaini majangili walipo kwavili mwendo wake ni mdogo." alifafanua Eric.

Aidha Eric alisema mbali na hilo ndege hiyo pia inatumia petroli hivyo ni ya gharama nafuu zaidi kuliko ndege za kawaida.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa na Rubani wa ndege aina ya Micro Light Nyinja, muda mfupi kabla ya kukabidhiwa ndege hiyo. Ndege hiyo ambayo imenunuliwa na kampuni ya Tanganyika Wildlife Safari ilikabidhwa kwa Waziri Nyalandu kwaajili ya kufuatilia majangili kwenye hifadhi za taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazari Nyalandu akizungumza jambo mara baada ya kukabidhiwa ndege aina ya Micro Light Nyinja, 5H-HEL, na Mwenyekiti wa Kampuni ya Utalii ya Tanganyika Wildlife Safari, Eric Pasanisi (kulia), werngine ni Askari wa kikosi cha wanyamapori walio hudhuria makabidhiano hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazari Nyalandu (kushoto) akikabidhiwa ndege aina ya Micro Light Nyinja, 5H-HEL, na Mwenyekiti wa Kampuni ya Utalii ya Tanganyika Wildlife Safari, Eric Pasanisi, werngine ni Askari wa kikosi cha wanyamapori walio hudhuria makabidhiano hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...